qurani tukufu - Ukurasa 11

IQNA

IQNA – Umoja wa Makari na Wahifadhi wa Qur’ani Tukufu nchini Misri umetangaza kuundwa kwa kamati maalum itakayoshughulikia ufuatiliaji wa utendaji wa makari na kushughulikia malalamiko yanayohusu usomaji wao.
Habari ID: 3481602    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/02

IQNA – Fainali ya mashindano ya kimataifa kuhifadhi Qur’ani kwa wanaume imeanza leo jijini Nairobi, Kenya.
Habari ID: 3481601    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/01

IQNA – Spika wa Bunge la Lebanon, Nabih Berri, amemkabidhi nakala ya Qur’ani Tukufu Papa Leo XIV, katika kikao chake na kiongozi wa Kanisa Katoliki aliyeko ziarani nchini humo.
Habari ID: 3481596    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/01

IQNA-Msikiti Mkuu wa Algiers umetangaza utayari wa kupokea wanafunzi wa kimataifa wa shahada ya uzamivu (PhD) katika Shule ya Juu ya Sayansi za Kiislamu (Dar-ul-Quran).
Habari ID: 3481593    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/30

IQNA – Mohamed Ameur Ghedira alikuwa profesa mashuhuri katika Chuo Kikuu cha Lyon aliyetarjumu Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kifaransa.
Habari ID: 3481591    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/30

IQNA – Wageni wa Maonyesho ya 48 ya Vitabu Kimataifa mjini Kuwait wamepewa zawadi ya nakala zaidi ya 5,000 za Qur'ani Tukufu. Banda la Wizara ya Mambo ya Kiislamu ya Saudi Arabia limesambaza nakala hizo, kwa mujibu wa taarifa ya Al-Madinah.
Habari ID: 3481590    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/30

IQNA – Toleo la 28 la Tuzo ya Qur’ani Tukufu na Sunna ya Sharjah limeingia hatua ya mwisho mjini Sharjah, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Habari ID: 3481587    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/29

IQNA – Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameeleza kuwa aya za Qur’ani Tukufu ni mwaliko wa tafakuri ya kina na mwanga wa hekima unaoweza kuangaza maisha na mwenendo wa binadamu.
Habari ID: 3481585    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/29

IQNA-Mkutano wa kielimu wa Qur’anI Tukufu uliopewa jina “Bibi Fatima Zahra (SA) na Sheria za Uteuzi wa Kimaumbile” umefanyika katika jimbo la Diyala, Iraq ukiratibiwa na Jumuia ya Kisayansi ya Qur’an chini ya usimamizi wa Haram ya Abbas (AS).
Habari ID: 3481583    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/28

IQNA – Marehemu Abdul Basit Abdul Samad, msomaji maarufu wa Qur’ani kutoka Misri na ulimwengu wa Kiislamu, ameheshimiwa katika kipindi cha televisheni cha Dawlet El Telawa nchini Misri
Habari ID: 3481572    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/26

IQNA – Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano ya kwanza ya kimataifa ya Qur’ani nchini Pakistan amesema anatarajia ushindani mkali katika mashindano hayo.
Habari ID: 3481571    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/26

IQNA – Televisheni ya Al-Kawthar imeanza maandalizi ya kuandaa toleo jipya la mashindano yake ya Qur’ani Tukufu yanayorushwa moja kwa moja yanayo julikana kama , “Inna lil-Muttaqeena Mafaza” (Hakika wachamungu watapata mafanikio).
Habari ID: 3481570    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/26

IQNA-Mahmoud Al-Toukhi, msomaji mashuhuri wa Qur’ani kutoka Misri, ametoa nakala ya usomaji wake wa Tarteel kwa Idhaa ya Qur’ani ya Kuwait.
Habari ID: 3481569    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/26

IQNA – Kipindi cha televisheni cha Qur’ani Tukufu nchini Misri, “Dawlet El Telawa”, kimepata mafanikio makubwa baada ya kurushwa sehemu nne pekee.
Habari ID: 3481568    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/26

IQNA – Mashindano ya kwanza ya kimataifa ya usomaji wa Qur'ani nchini Pakistan yameanza rasmi Jumatatu katika mji mkuu wa Islamabad.
Habari ID: 3481566    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/25

IQNA – Jumamosi iliyopita, kikao cha kuandaa hati ya makubaliano ya ushirikiano katika shughuli za Qur'ani Tukufu kati ya Mkoa wa Khuzestan nchini Iran na Mkoa wa Basra nchini Iraq kimefanyika mjini Basra.
Habari ID: 3481563    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/25

IQNA – Maonyesho ya pili ya kazi za Qur’ani Tukufu zilizotengenezwa kwa teknolojia ya Akili Mnemba (AI) yamezinduliwa mjini Tehran, yakionyesha kazi 100 zilizochaguliwa kutoka kwa vijana na chipukizi.
Habari ID: 3481562    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/23

IQNA – Vikundi vya usomaji Qur’an katika misikiti ya Mkoa wa Kaskazini mwa Sinai, Misri, vimepokelewa kwa shangwe na raia wa Kimasri.
Habari ID: 3481561    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/23

IQNA-Hatua ya mwisho ya Mashindano ya Qur’an ya Sheikh Jassim bin Mohammed bin Thani, toleo la 30, inaendelea mjini Doha, Qatar ikihusisha mashindano ya wazi kwa wahifadhi kamili na sehemu.
Habari ID: 3481558    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/23

Istighfar Katika Qur’ani Tukufu / 1
IQNA-Katika aya za Qur’ani Tukufu na Hadith za Maimamu Maasumu (amani iwe juu yao), Istighfar , yaani kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, imepewa msisitizo mkubwa na kutambulishwa kwa upekee.
Habari ID: 3481556    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/22