TEHRAN (IQNA) – Shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani amezikwa kwa kuchelewa kufuatia msongamano mkubwa katika mji wa Kerman kusini mashariki mwa Iran.
Habari ID: 3472347 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/07
TEHRAN (IQNA) - Chama tawala cha ANC cha Afrika Kusini kimetoa taarifa rasmi na kulaani hujuma ya Jeshi la Markeani ambayo ilipelekea kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC)
Habari ID: 3472346 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/06
TEHRAN (IQNA) -Bintiye Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani zifahamu kuwa, kuuawa shahidi baba yake kutibua mwamko mkubwa na kuimarisha harakati za mapambano au muqawama katika eneo.
Habari ID: 3472342 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/06
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amefika Tehran kushiriki katika shughuli ya mazishi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na mashahidi wenzake.
Habari ID: 3472341 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/06
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Mashia wa Iraq, Ayatullah Sayyed Ali al-Sistani amemtumia risala ya rambirambi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei kufuatia kuuawa shahidi kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Liteni Jenerali Qassem Soleimani.
Habari ID: 3472338 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/05
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, tarehe 3 Januari 2020 ambayo ni siku ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, ni mwanzo wa historia mpya katika eneo la Asia Magharibi.
Habari ID: 3472337 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/05
TEHRAN (IQNA) - Mwili mtoharifu wa Shahidi Luteni Jenerali Haj Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) umewasili katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema leo asubuhi katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Ahwaz kusini mwa nchi.
Habari ID: 3472336 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/05
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani amesema: Jina la Luteni Jenerali Qassem Soleimani litaheshimika na kubakia milele katika historia ya taifa la Iran na wapigania uhuru duniani.
Habari ID: 3472334 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/04
TEHRAN (IQNA) – Wananchi wa Nigeria wamendamana kulaani jinai ya Marekani ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
Habari ID: 3472332 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/04
Kufuatia dikrii ya Kiongozi Muadhamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Iran amemteua Brigedia Jenerali Esmail Qaani kuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
Habari ID: 3472331 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/04
Khatibu wa Sala ya Ijumaa
TEHRAN (IQNA) - Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ameashiria juu ya kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kusisitiza kuwa, Wamarekani katu hawataonja tena ladha ya amani popote duniani kufuatia ukatili huo.
Habari ID: 3472330 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/03
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma salamu za rambirambi kutokana na kuuliwa shahidi Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Suleimani na kusema kuwa: Kisasi kikali kinawasubiri watenda jinai ambao mikono yao michafu imemwaga damu yake na mashahidi wengine katika shambulizi la usiku wa kuamkia leo.
Habari ID: 3472329 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/03
TEHRAN (IQNA) - Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Luteni Jenerali Qassem Suleimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes wameuawa shahidi mapema leo Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika barabara ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.
Habari ID: 3472328 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/03
TEHRAN (IQNA) – Maelfu ya watu wa India wameukaribisha mwaka mpya wa 2020 Miladia kwa maandamano ya kupinga sheria ya uraia inayowabagua Waislamu.
Habari ID: 3472327 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/02
TEHRAN (IQNA) – Ubalozi wa Marekani mjini Baghdad nchini Iraq, Jumatnao ulitangaza kusitisha huduma zote kwa umma kufuatia maandamano ya wananchi waliokuwa na hasira wa Iraq nje ya ubalozi huo.
Habari ID: 3472326 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/02
TEHRAN (IQNA) – Mwanamke Mwislamu nchini Marekani ametimuliwa katika mgahawa aliokuwa akifanya kazi kwa sababu tu ya kuja kazini akiwa amevalia vazi la staha la Hijabu.
Habari ID: 3472325 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/02
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinzudi ya Kiislamu akibainisha kwamba, 'Mimi, serikali na taifa la Iran tunalaani vikali shambulizi la Marekani dhidi ya Hashdu sh-Sha'abi ya Iraq', amesisitiza kuwa, watu wa eneo hili wanaichukia sana Marekani.
Habari ID: 3472324 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/01
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia ujumbe wa pongezi marais na viongozi na mataifa ya Wakristo kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa Miladia wa 2020.
Habari ID: 3472323 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/01
TEHRAN (IQNA) – Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi Wapalestina 149 katika mwaka uliopita wa 2019, aghalabu wakiwa katika Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3472322 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/01
TEHRAN (IQNA) – Idara ya Kufuatia Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) katika Chuo cha Al Azhar nchini Misri imelaani hatua mwanasiasa mwenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Uholanzi ya kupanga kufanyika mashindano ya vibonzo vya kumdhalilisha Mtume Muhammad SAW.
Habari ID: 3472321 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/31