iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Mkurugenzi wa Kitengo cha Kimataifa cha Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran amesema kushirikiana na taasisi za kimataifa za Qur'ani ni moja kati ya malengo muhimu ya maonyesho ya mwaka huu.
Habari ID: 3471959    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/05/16

TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa Iran ya Kiislamu wameandamana nchi nzima baada ya Sala ya Ijumaa kuunga mkono hatua zilizochukuliwa na serikali ya Iran kusimamisha utekelezaji wa baadhi ya ahadi zake katika mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA).
Habari ID: 3471950    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/05/10

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha majukumu ya Hawza (vyuo vikuu vya kidini) na maulamaa katika kubainisha maarifa ya Uislamu na kufanya juhudi kwa ajili ya kufikiwa hilo katika jamii na kusisitiza kwamba, maulamaa wakiwa warithi wa Manabii wanapaswa kufanya hima kubwa ili tawhidi na uadilifu vipatikane kivitendo katika jamii.
Habari ID: 3471949    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/05/09

TEHRAN (IQNA) -Iran imesimamisha kwa muda utekelezaji wa baadhi ya ahadi zake kuhusu mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA), ikiwa ni mwaka mmoja baada ya Marekani kujitoa kwa upande mmoja katika mapatano hayo muhimu ya kimataifa.
Habari ID: 3471946    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/05/08

TEHRAN (IQNA)- Hatua ya serikali ya Marekani kuiwekea Iran vikwazo vya mafuta baada ya kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA imekabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wanunuzi wa mafuta ghafi ya petroli ya Iran katika soko la kimataifa na pia kutoka kwa wakuu wa Shirika la Nchi Zinazouza Mafuta kwa Wingi Duniani (OPEC).
Habari ID: 3471940    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/05/04

TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema leo Jumatano wakati huu wa kukaribia maadhimisho ya Siku ya Mwalimu nchini Iran kwamba kama taifa litashikamana na kuwa kitu kimoja, basi njama zote za adui zitamrudia mwenyewe.
Habari ID: 3471938    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/05/02

Rais Hassan Rouhani
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Iran Jamhuri ya Kiislamu amesema nchi hii katu haitasitisha uuzaji wa mafuta ghafi yake ya petroli katika soko la kimataifa pamoja na kuwepo mashinikizo na vikwazo vipya vya Marekani.
Habari ID: 3471936    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/30

TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kundi lenye misimamo mikali la Timu B linamchochea Rais Donald Trump wa Marekani aanzishe vita dhidi ya Iran.
Habari ID: 3471932    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/29

Spika wa Bunge la Iran
TEHRAN (IQNA) -Spika wa Bunge la Iran, Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, ulimwengu wa Kiislamu leo unakabiliwa na tatizo la misimamo mikali na utakfiri.
Habari ID: 3471931    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/28

TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, uhusiano wa mataifa mawili ya Iran na Pakistan ni wa moyoni uliokita mizizi vyema na kusisitiza kuwa, uhusiano huo unapaswa kuimarishwa kadiri inavyowezekana hata kama maadui wa mataifa haya mawili watachukizwa na hilo
Habari ID: 3471924    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/23

TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran maalumu kwa ajili ya wanawake yamemalizika Ijumaa mjini Tehran.
Habari ID: 3471914    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/13

TEHRAN (IQNA)- Harakazi za mapambano ya Kiislamu Iraq ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi zimelaani vikali, hatua ya uhasama ya mtawala wa Marekani Donald Trump ya kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) nchini Iran katika orodha ya makundi ya kigaidi.
Habari ID: 3471910    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/11

TEHRAN (IQNA)- Fainali za Mashindano ya 36 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimeanza rasmi Jumatano alasiri katika halfa iliyofanyika mjini Tehran.
Habari ID: 3471909    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/10

TEHRAN (IQNA) – Nchi 27 zitawakilishwa katika Mashindano ya 6 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa shule.
Habari ID: 3471905    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/08

TEHRAN (IQNA) – Washiriki wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wameanza kuwasili nchini.
Habari ID: 3471904    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/08

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Marekani inapinga mchakato wa demokrasia nchini Iraq.
Habari ID: 3471903    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/07

Kiongozi wa Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwepo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika harakati ya Tauhidi (Kumpwekesha Mwenyezi Mungu) ni chanzo kikuu cha uhasama wa Marekani na vibaraka wake kama vile ukoo wa Aal Saud.
Habari ID: 3471897    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/03

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika ujumbe kwa munasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1398 Hijiria Shamsia, ametuma salamu za pongezi za Nowuruz (Nairuzi) na pia salamu kwa munasaba Wilada ya Imam Ali AS kwa wananchi wa Iran na hasa familia za mashahidi na majeruhi wa vita na amelitakia taifa la Iran mwaka wenye furaha, saada, afya ya kimwili na mafanikio ya kimaada na kimaanawi na ameutaja mwaka mpya kuwa mwaka wa "kustawi uzalishaji".
Habari ID: 3471884    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/21

Rais Rouhani katika ujumbe wa Nowruz
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema Alhamisi ametuma ujumbe kwa kunasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1398 Hijria Shamsiya na kusema mwaka 1397 ulikuwa mwaka wa mafanikio makubwa ya taifa la Iran katika nyuga mbali mbali na kuongeza kuwa, kwa yakini taifa la Iran litapata ushindi na litavuka matatizo yaliyopo.
Habari ID: 3471883    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/21

TEHRAN (IQNA)-Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali hujuma za kigaidi zilizolenga misikiti miwili jana mjini Christchurch New Zealand na kupelekea Waislamu wasiopungua 49 kuuawa shahidi wakiwa katika Sala ya Ijumaa.
Habari ID: 3471878    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/16