TEHRAN (IQNA)- Ujumbe wa utawala wa Kizayuni wa Israel unaripotiwa kuitembelea Sudan kwa siri na kificho, muda mfupi baada ya kujiri mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika Oktoba 25 mwaka huu katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Habari ID: 3474510 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/03
TEHRAN (IQNA)- Walowezi za Kizayuni wameendeleza hujuma zao dhidi ya msikiti wa Al Aqsa katika mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3474499 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/01
TEHRAN (IQNA) Kwa mara nyingine, Utawala wa Kizayuni wa Israel unawazuia Waislamu Wapalestina kuingia Msikiti wa Nabii Ibrahim AS katika mji wa Al Khalil (Hebron) ulio katika eneo Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, linalokaliwa kabavu na utawala huo ghasibu.
Habari ID: 3474497 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/31
TEHRAN (IQNA)- Sherehe kubwa imefanyika Jumatano usiku katika Ukanda wa Ghaza huko Palestina kuwaenzi wasichana na wavulana 1,000 ambao wamehifadhi Qur'ani hivi karibuni.
Habari ID: 3474489 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/29
TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Ulaya (EU) umekariri wito wake kwa utawala haramu wa Israel usitishe mpango wake wa kujenga vitongoji zaidi vya walowezi wa Kizayuni katika mji wa Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3474486 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/29
TEHRAN (IQNA)- Makundi ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina yameuonya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kuhusiana na kuendelea uvamizi na hujuma dhidi ya maeneo matakatifu ya Kiiislamu huko Palestina hususan maziara makaburi ya al-Yusufiya huko Quds (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Habari ID: 3474480 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/27
TEHRAN (IQNA)- Kwa mara ya kwanza, ndege ya moja kwa moja kutoka Ufalme wa Saudi Arabia inatazamiwa kutua leo Jumatatu usiku katika katika utawala bandia wa Israel.
Habari ID: 3474469 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/25
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imepongeza tamko la Waziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia ambaye amesema nchi yake katu haitaanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3474451 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/21
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Algeria ameelezwa kusikitishwa kwake na hatua ya baadhi ya nchi ya kung'ang'ania utawala haramu wa Israel upatiwe hadhi ya mwanachama mwangalizi katika Umoja wa Afrika.
Habari ID: 3474431 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/16
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imetangaza kuwa nchi hiyo inapinga utawala wa Kizayuni wa Israel kupewa hadhi ya mwanachama mwangalizi katika Umoja wa Afrika.
Habari ID: 3474424 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/15
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu (OIC) imelaani vikali kitendo cha utawala haramu wa Israel cha kubomoa maziara au makaburi ya Waislamu katika mji wa Quds, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Habari ID: 3474417 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/13
TEHRAN (IQNA) Harakati ya Jihad Islami ya kupigania ukombozi wa Palestina imefanya maadhimisho kwa mnasaba wa kutumia mwaka wa 34 tangu kuasisiwa kwake.
Habari ID: 3474402 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/09
TEHRAN (IQNA) Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi ameutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka za kuhitimisha jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya Palestina.
Habari ID: 3474376 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/03
TEHRAN (IQNA)- Harakati kadhaa za kupigania ukombozi wa Palestina zimelaani vikali hatua ya ufalme wa Bahrain kumpokea waziri wa mambo ya nje wa utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3474372 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/02
TEHRAN (IQNA)- Watu wa Bahrain wamefanya maandamano makubwa katika miji kadhaa ya nchi hiyo kupinga waziri wa mambo ya nje wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kukanyaga ardhi ya nchi yao na kuanzishwa uhusiano wa kawaida na Tel Aviv.
Habari ID: 3474366 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/01
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) Ismail Haniya amesema rais Joe Biden wa Marekani na Naftali Bennet waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel hawaafiki utatutzi wowote wa kisiasa wa kadhia ya Palestina.
Habari ID: 3474365 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/30
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS kwa mara nyingine tena imeishukuru serikali, makundi ya kisiasa, wazee wa koo na viongozi wa makabila ya Iraq, kwa msimamo wao wa kupinga kuanzishwa mapatano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3474355 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/28
TEHRAN (IQNA)- Mkutano mkuu wa chama cha Leba nchini Uingereza umepigia kura na kupitisha hoja ya kuitambua Israel kuwa ni utawala unaotenda jinai ya ubaguzi wa Apathaidi, na kukifanya kuwa chama cha kwanza kikubwa cha siasa barani Ulaya kuchukua msimamo huo dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni.
Habari ID: 3474349 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/27
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, hii leo mapambano na muqawama ni upanga na ngao ya wananchi wa Palestina na kwamba, taifa la Palestina limeazimia na kukusanya nguvu zake kwa ajili ya ukombozi wa ardhi yake.
Habari ID: 3474345 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/26
TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi wa utawala dhalimu wa Israel wamemuua Mpalestina aliyekuwa katika maandamani ya amani ya kupinda ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Habari ID: 3474342 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/25