IQNA

Misahafu ya kale yazawadiwa Akademia ya Qur’ani Sharjah

19:36 - August 23, 2021
Habari ID: 3474220
TEHRAN (IQNA)- Sheikh Sultan Bin Mohammed Al Qasimi, Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Mtawala wa Sharjah, amekabidhi nakala nne nadra za nakala za Qur'ani Tukufu kwa Akademia ya Qur'ani Tukufu mjini Sharjah.

Misahafu hiyo imetajwa kuwa kati ya hazina muhimu za akiolojia ambazo zinaongezwa kwa umiliki wa Akademia ya Qur'ani Tukufu na hivyo kuwapa wageni na watafiti wa  nafasi ya kuiona, kujifunza kuhusu historia , na kufanya utafiti .

Misahafu hiyo nadra ni ya kutoka kipindi cha watawala wa Iran wa silsila ya Ilkhanid katika karne ya saba Hijria Qamaria. Misahafu inanasibishwa na  mwandishi hati maarufu Yaqut Al Musta'simi.

Hati hiyo iliandikwa kwa maandishi makubwa ya thuluth, na mapambo ya lapis lazuli, pamoja na tafsiri ya Kiajemi au Kifarsi ya Qur’ani Tukufu.

Hidaya ya pili ya msahafu wa pili nadra  adimu ni ile ya karne ya 2 Hijri.

Hati hiyo iliandikwa katika maandishi yasiyo na alama au ‘harakat’ na  wino mwekundu umetumika katika maandishi.

Msahafu wa tatu ni ule ulioandikwa kwenye ngozi ya kulungu katika zama za watawala wa Bani Abbas na  inakadiriwa kuwa kati ya mwisho wa karne ya pili na mwanzoni mwa karne ya tatu Hijria, kwa kutumia mbinu ya kale ya maandishi ambayo ilitumiwa na Al Khalil Bin Ahmed Al Farahidi.

Zawadi ya nne ni ya misahafu miwili ilivyoandikwa mnamo 780 Hijria, na ina mapambo ya lapis lazuli.

3475561

Kishikizo: sharjah ، misahafu ، qurani tukufu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha