IQNA

Kusambaratika Israel

Kiongozi wa Hizbullah anukulu Qur’ani kuashiria kuangamia utawala wa Israel

14:13 - March 28, 2023
Habari ID: 3476773
TEHRAN (IQNA) – Akiashiria sehemu ya aya ya 2 ya Sura Al Hashr katika Qur’ani Tukufu, naibu kiongozi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amegusia mgogoro mkubwa katika utawala haramu wa Israel na kuandika: “Wakawa wanazibomoa nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini.”

Kwa mujibu wa Al-Manar, Sheikh Naim Qassem, Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amenukuu aya ya Qur'ani Tukufu na kusisitiza kuwa, Utawala wa Muda wa Kizayuni uko kwenye hatihati ya kudidimia na kuangamizwa.

Ameandika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter: "Mbegu ya mwisho ya kungamia utawala unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina imepandwa ndani ya utawala huu, na haijalishi itadumu kwa muda gani, kwani kwa subira, Jijadi na kujitolea taifa la Palestina hakuna shaka kuwa utawala wa Kizayuni utaangamia." Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria pia aya ya 2 ya Surat al-Hashr isemayo, يُخْرِبُونَ بُيُوتَهُمْ بِأَيْدِيهِمْ وَأَيْدِي الْمُؤْمِنِينَ " wanazibomoa nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini.”

Ameongeza kuwa utawala wa Kizayuni bila shaka utaangamizwa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu.

Maelfu ya walowezi wa Kizayuni wameandamana kwa wiki 11 mfululizo kupinga mpango wa mageuzi ya mahakama unaoshinikizwa na Waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu. Mageuzi hayo yalikuwa na lengo la kulipa bunge kauli ya mwisho kuhusu hukumu zinazotolewa na mahakama. Netanyahu amekuwa akipigia debe mageuzi hayo kwa sababu anakabiliwa na kesi kadhaa za ufisadi.

Hatimaye Netanyahu amelazimika kutupilia mbali mageuzi hayo lakini Pamoja na hayo mustakabali wa utawala wa Kizayuni uko matatani na weledi wengi wa mambo wanaamini kuwa utawala huo uko katika mkondo wa kuangamia.

4130230

captcha