IQNA

Al-Azhar kuwasilisha machapisho ya Qur'ani na Kiislamu katika Maonyesho ya Vitabu ya Cairo 

18:52 - January 15, 2025
Habari ID: 3480058
IQNA – Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kitawasilisha machapisho yake mapya katika toleo la 56 la Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo.

 

Kituo cha Al-Azhar, chini ya usimamizi wa kiongozi wake Sheikh Ahmed Al-Tayyeb, kitashiriki katika maonyesho hayo ya vitabu kwa kuweka banda lake maalum.

Tukio hilo la kimataifa la kitamaduni litafanyika katika mji mkuu wa Misri kuanzia Januari 23 hadi Februari 5, 2025, kwa mujibu wa tovuti ya al-Mashhad.

Kwa mwaka wa tisa mfululizo, banda la Al-Azhar litakuwepo kwenye maonyesho hayo ya vitabu, yanayofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Maonyesho na Mikutano cha Misri. 

Vitabu ya Sheikh Alim Muhammad Abdullah Daraz, mhitimu wa Al-Azhar na Sorbonne nchini Ufaransa, na mwandishi wa kitabu “Sheria ya Katiba ya Maadili katika Quran”, vitaonyeshwa kwenye banda hilo kwa lugha ya Kifaransa na Kiarabu. 

Al-Azhar itawasilisha mkusanyiko kamili wa machapisho yake ili kukidhi mahitaji ya washiriki Wamisri na wageni wa maonyesho hayo. 

Katika maonyesho hayo Al Azhar itazindua juzuu ya pili ya kitabu cha Kiarabu “Watoto Wanauliza Sheikh wa Al-Azhar,” pamoja na tafsiri za Kiingereza na Kifaransa za juzuu ya kwanza, ambayo imepokelewa vyema na watoto na wazazi.  

3491455

Habari zinazohusiana
captcha