Hoja hiyo, iliyowasilishwa katika Bunge la Uskochi na James Dornan, ililaani uanachama wa Israel katika vyama vya michezo vya Ulaya, ikizitaka taasisi husika kufuta ushiriki wake mara moja.
Hoja hiyo ilinukuu mitazamo inayobaini kuwa kuwa sera ya utawala wa Israel ni ya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza. Hoja hiyo pia ilieleza kuwa “utekelezaji wake wa sera hiyo kikatili na ba bila huruma ni sababu tosha ya kuondolewa kwa Israel kutoka vyama vya michezo vya Ulaya.”
Dornan alizitaka taasisi kama vile Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA), Shirikisho la Mpira wa Kikapu Ulaya, Shirikisho la Mpira wa Mikono Ulaya, na Shirikisho la Riadha Ulaya kuchukua hatua ya haraka ya kuiondoa Israel.
Mwezi uliopita, Francesca Albanese, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu katika maeneo ya Palestina, alitoa wito kwa UEFA kuifukuza Israel kutoka mashindano kwa kuwa utawala huo umehusika katika uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika Ukanda wa Gaza.
Utawala wa Israel umeendeleza mashambulizi ya kikatili dhidi ya Gaza, ambapo takriban Wapalestina 64,700 wameuawa tangu Oktoba 2023. Kampeni hiyo ya kijeshi imeharibu kabisa eneo hilo, ambalo sasa linakabiliwa na baa la njaa.
Hadi sasa kuna mashahidi 774 kutoka miongoni mwa jamii ya wanamichezo, ikiwa ni pamoja na wachezaji wa mpira wa miguu 355, wanachama 277 wa mashirikisho ya michezo, 142 kutoka Harakati ya Skauti ya Palestina na 15 kutoka Muungano wa Vyombo vya Habari vya Michezo. Pia, wanariadha 119 wametoweka na viwanja 288 vya michezo katika Ukingo wa Magharibi na Gaza vimeharibiwa kabisa au kwa sehemu fulani. Kulingana na Rajoub, baadhi ya maeneo haya, kama vile Uwanja wa Palestina na Yarmouk, yamekuwa makazi ya watu waliokimbia makazi yao.
Mwezi Novemba uliopita, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wake wa zamani wa vita Yoav Gallant kwa tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu huko Gaza.
Aidha, Israel inakabiliwa na kesi ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutokana na vita vyake dhidi ya Gaza.
3494564