IQNA

Uwezo wa Teknolojia za Maarifa ya Qur’ani wajitokeza katika Maonesho ya Qur’ani Tehran

14:34 - February 25, 2026
Habari ID: 3481993
IQNA – Mkurugenzi wa Sehemu ya Akili Unde au Akili Mnemba (Artificial Intelligence) na Teknolojia za Maarifa ya Qur’ani katika Maonesho ya 33 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Tehran amesema kuwa, licha ya uwepo mdogo wa makampuni ya maarifa, mchango wao ni wa kimkakati na wenye athari kubwa.

Katika mahojiano na IQNA, Seyed Yasser Sajedi alitangaza uzinduzi wa chatbot za Qur’ani, kuandaliwa kwa mashindano ya uzalishaji wa maudhui kwa kutumia AI, pamoja na vikao maalumu vya kielimu vya taaluma mseto ndani ya sekta hiyo.

“Katika miaka ya karibuni, mfumo wa ikolojia wa maarifa ya Qur’ani nchini Iran umejengeka na kufikia kiwango muhimu cha uwezo. Lengo letu katika toleo hili la maonesho ni kuyafanya uwezo haya yaonekane kwa vitendo, yawasilishwe kwa jamii, na kutambulisha bidhaa na huduma za Qur’ani zinazotegemea maarifa,” alisema Sajedi.

Akirejelea idadi ndogo ya makampuni ya maarifa ya Qur’ani, aliongeza:

“Kati ya taasisi 4,000 hadi 5,000 za Qur’ani zinazofanya kazi nchini, chini ya makampuni 20 pekee ndiyo yamepata hadhi ya ‘maarifa’ kupitia Wizara ya Sayansi na Teknolojia. Bila shaka, si makampuni yote yaliweza kushiriki katika maonesho haya kwa sababu mbalimbali, hususan changamoto za kiuchumi; hata hivyo, kila kampuni iliyotangaza utayari wake ilipewa fursa ya kushiriki.”

Sajedi pia alisema kuwa juhudi zimefanywa kutambulisha bidhaa bunifu za makampuni ambayo hayakuweza kuhudhuria maonesho kwa njia mbalimbali.

 Akili Mnemba Katika Huduma ya Qur’ani

Akizungumzia programu zinazohusiana na akili unde, Sajedi alisema:

“Mwaka huu tulijitahidi kuleta kitu tofauti katika uwanja wa AI; hata hivyo, uwezo wa teknolojia hii katika nyanja ya Qur’ani na Ahlul‑Bayt (AS) ni mkubwa zaidi kuliko uwezo wetu wa sasa.”

Alieleza kuwa shughuli za AI katika uwanja huu zinaelekezwa katika mwelekeo miwili:

1.Kutengeneza Zana za AI kwa Huduma ya Qur’ani

Hii ni pamoja na kubuni chatbot maalumu za Qur’ani zinazoweza kujibu maswali ya Qur’ani kwa njia ya akili na uelewa wa kisasa. Sehemu hii inasimamia uundaji wa zana za vitendo zinazotegemea akili unde.

2. Kutumia AI Zalishi (Generative AI) kwa Uzalishaji wa Maudhui

Katika mwelekeo huu, tukio la uzalishaji wa maudhui ya Qur’ani limeandaliwa, likiwahusisha vijana na balehe wanaoshiriki kwa makundi ya watu 4 hadi 5 kila jioni kuanzia saa 1:00 usiku hadi saa 5:00 usiku.

 “Kwa wastani, washiriki 60 hadi 70 hushiriki kila usiku, wakiwa wamegawanyika katika takriban timu 15,” alisema.

Vikao vya Kielimu na Taaluma Mseto

Aidha, Sajedi alisema kuwa vikao vya kisayansi vya taaluma mseto vimeandaliwa ili kuchunguza uhusiano kati ya akili unde na tafiti za Qur’ani.

Katika vikao hivyo, mada kama:

  • uhusiano wa AI na tafiti za Qur’ani,
  • matumizi ya chatbot katika masomo ya dini,
  • na vipengele vya kinadharia na kivitendo vya teknolojia hii,

vinajadiliwa kwa kina.

Alimalizia kwa kusisitiza:

 “Lengo letu kuu ni kuonesha kuwa teknolojia za kisasa, hasa akili unde, zinaweza kuitumikia Qur’ani Tukufu na mafundisho ya Ahlul‑Bayt (AS), na kufungua milango ya ubunifu, uzalishaji wa maudhui, na uenezaji wa utamaduni wa Qur’ani miongoni mwa kizazi cha vijana.”

Maonesho haya yanaendelea hadi tarehe 6 Machi, yakibeba kaulimbiu:

“Iran chini ya Ulinzi wa Qur’ani.”

Maonesho ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Tehran huandaliwa kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na Wizara ya Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu ya Iran.

Kwa kuwa na programu mbalimbali kama:

  • vikao maalumu vya kielimu,
  • warsha za mafunzo,
  • mikusanyiko ya Qur’ani,
  • na shughuli mahsusi kwa watoto na vijana,

maonesho haya yanalenga kueneza mafundisho ya Qur’ani na kuonesha mafanikio ya hivi karibuni ya Qur’ani nchini Iran, pamoja na bidhaa na huduma zinazohudumia Kitabu Kitukufu.

 3496552

captcha