IQNA

Uchambuzi wa Mapambano Dhidi ya Uzayuni katika Qur’ani / 15

Mantiki ya Qur’ani Kuhusu Kujibu Uadui na Uchokozi wa Adui

18:26 - March 25, 2026
Habari ID: 3482089
IQNA – Serikali ya Kiislamu haianzi vita dhidi ya yeyote, lakini ina wajibu wa kujibu uchokozi, fitina na vitendo vya kueneza hofu ili msaada wa Mwenyezi Mungu uweze kuifikia.

Qur’ani Tukufu inaweka masharti matatu kuhusu kupigana na adui:

“Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.” (Aya ya 190 ya Surah AlBaqarah).

Kwanza, vita vinapaswa kuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na katika njia Yake. Pili, viwe dhidi ya yule anayefanya uchokozi; na maadamu vita havijalazimishwa, mtu asichukue silaha. Tatu, hata katika uwanja wa vita, haifai kuvuka mipaka bali lazima kuzingatia misingi ya maadili.

Kwa msingi huo, kuitetea Iran ya Kiislamu katika vita vilivyolazimishwa dhidi yake na utawala wa Kizayuni pamoja na Marekani kunachukuliwa kuwa kitendo halali na kinacholingana na mafundisho ya Qur’ani.

Katika aya zinazofuata, Qur’ani inaeleza namna ya kujibu:

“Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu..” (Aya ya 194 ya Surah AlBaqarah).

Uislamu unampa kila mtu haki ya kujibu kwa namna inayolingana iwapo amefanyiwa uchokozi. Kwa mfano, iwapo adui atavamia ardhi ya nchi ya Kiislamu kutoka nchi nyingine, kuna haki ya kujibu kwa kulenga maslahi ya yule anayefanya uchokozi.

Kwa mfano, ikiwa mitambo ya kusafisha mafuta na gesi ya Iran itashambuliwa kwa mabomu, Iran inaweza kisheria kulenga maslahi na uwekezaji wa wanaotoa vituo au misaada kwa adui, kama hatua ya adhabu na kuzuia uchokozi zaidi.

Uchokozi unalaumiwa pale unapokuwa wa kuanzisha, si pale unapokuwa ni majibu ya uchokozi wa wengine. Jamii ambayo haiko chini ya dhuluma, utumwa au udhalilishaji inapojibu uchokozi wa wengine, kitendo hicho huonekana kuwa ni fadhila kubwa; kwa sababu kunyenyekea kwa mchokozi ni sawa na kufa, ilhali kusimama na kupinga ni sawa na uhai.

3496827

Kishikizo: uzayuni qurani tukufu
captcha