IQNA

Kashfa ya kuwa kuwakejeli wachezaji Waislamu Uhispania

21:39 - April 15, 2026
Habari ID: 3482141
IQNA – Kile kilichoanza kama mzaha wa kistaarabu wa “Siku ya Wajinga wa Aprili” hatimaye kimegeuka kuwa kashfa iliyoangusha uongozi wa rais wa klabu moja ya daraja la chini nchini Uhispania.

Soka la Hispania limetikiswa na sintofahamu mpya baada ya video kuonyesha rais wa klabu ya ngazi za chini akiwafukuza wachezaji Waislamu huku akiwa amebeba bidhaa za nyama ya nguruwe, jambo lililozua hasira na kumlazimu kujiuzulu.

Tukio hilo limezidisha mjadala kuhusu ubaguzi na utofautishaji ndani ya mchezo huo nchini Uhispania.

Sakata linamhusu Javi Poves, rais wa CD Colonia Moscardó, klabu kutoka Madrid inayocheza Ligi Daraja la Nne.

Katika video aliyopakia kwenye mitandao ya kijamii, na baadaye akaifuta, Poves alionekana akitangaza bidhaa za nyama ya nguruwe aina ya Iberian pork, kisha akiwafuatilia wachezaji Waislamu huku akiwapigia kelele wawale.

Video hiyo ilisambaa upesi mtandaoni na kukabiliwa na ukosoaji mkali kutoka kwa mashabiki, vyombo vya habari na watazamaji, wengi wakilichukulia tukio hilo kama dharau na ubaguzi, si mzaha.

Wakati wa tukio nao uliifanya hali kuwa tete zaidi, kwani soka la Uhispania tayari lilikuwa chini ya presha kufuatia matukio kadhaa ya hivi karibuni yanayohusisha ubaguzi wa rangi.

Poves alijaribu kupoza hali kwa kutoa video ya dakika tatu akieleza kuwa lilikuwa “tarehebahati iliyotafsiriwa vibaya”.

“Lilikuwa jaribio la kuleta ucheshi… sikuwa na nia ya kuikosoa dini yoyote au mtu yeyote,” alisema.

Hata hivyo, maelezo hayo hayakutuliza hali. Wakosoaji walisisitiza kuwa kitendo hicho kilivuka mipaka ya heshima na kuashiria kutokujali imani za wachezaji, na hivyo kuibua wito wa kuwajibika.

Chini ya shinikizo kubwa, Poves alitangaza kujiuzulu rasmi kama rais wa klabu, japokuwa amebaki kwenye bodi ya uongozi. Katika video yake ya mwisho, alidokeza kuacha kabisa shughuli za mpira wa miguu.

“Nitaanza ukurasa mpya katika maisha yangu… nitalima nyanya na kuwalea kondoo,” alisema.

Hadi sasa, Shirikisho la Soka la Hispania halijatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo licha ya kuongezeka kwa wito wa kufanyika uchunguzi.

3497074

Kishikizo: uhispania soka waislamu
captcha