IQNA

Msafara wa kwanza wa Wairani wanaolekea Hija wawasili Saudia

14:57 - April 25, 2026
Habari ID: 3482163
IQNA – Msafara wa kwanza wa Wairani wanaoshiriki katika Ibada ya Hija mwaka huu umewasili Saudi Arabia.

Katika hafla ya kuwaaga waumini hao iliyofanyika Tehran, afisa mkuu wa Hija nchini amesema kuwa mahujaji wa Iran, katika ardhi ya Wahyi, watakuwa mstari wa mbele katika kuimarisha umoja wa Ummah wa Kiislamu.

Hujjatul-Islam Sayyid Abdol Fattah Navab, mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi katika masuala ya Hijja na mkuu wa msafara wa Hijawa Iran, aliyasema hayo katika hafla ya kuwaaga kundi la kwanza la raia wa Iran wanaoelekea Hija mwaka huu wa 1447 Hijria Qamaria, iliyofanyika asubuhi ya Jumamosi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini (RA).

Amesema: “Pamoja na vita vya kichokozi vilivyolazimishwa dhidi ya nchi, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kulifungua lango la Nyumba Yake kwa Mahujaji tarajiwa waliokuwa wakisubiri kwa miaka mingi."

Akinukuu baadhi ya aya za Qur’ani kuhusu Hija, alisema kuwa Mahujaji wa Iran katika ardhi ya ufunuo watakuwa waanzilishi wa mipango ya Iran ya Kiislamu na umoja wa Ummah wa Kiislamu, na katika safari hii ya kiroho, bila shaka watawakumbuka wapendwa wao ambao hawakuweza kuhudhuria Hija.

Akizungumza na watumishi wanaoelekea ardhi ya ufunuo kuhudumia mahujaji wa Kiirani, Hujjatul-Islam Navab alisema: "Mmechukua jukumu tukufu la kuwatumikia mahujaji, na mnapaswa kulitekeleza jukumu hili kwa ikhlasi."

Akibainisha kuwa Hija ya mwaka huu ni tofauti na miaka iliyopita kutokana na kuondokewa na Imam aliyeuawa shahidi pamoja na idadi kubwa ya makamanda, maafisa, na wananchi, alitaja kwa heshima kumbukumbu ya Shahidi Alireza Bayat, aliyekuwa mkuu wa Shirika la Hija, akisema kuwa majina ya watu hawa yatakuwa mbebaji wa bendera ya Ummah wa Kiislamu duniani.

Aidha amekumbusha umuhimu wa umoja baina ya wananchi na viongozi, akasisitiza kuwa kila mmoja anapaswa kutenda na kutimiza wajibu wake kwa kuzingatia mwongozo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, na maagizo yake, ili kudumisha umoja.

3497216

Kishikizo: hija iran saudi arabia
captcha