IQNA – Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetaja baa la njaa linaloikumba Ukanda wa Gaza kuwa ni janga lililosababishwa na binadamu, ambalo linaweza kuzuilika na kurekebishwa endapo kutakuwepo na nia ya dhati ya kisiasa.
Habari ID: 3481208 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/09
IQNA – Akielezea unyama unaoendelea kufanywa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina, Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu amesisitiza haja ya kukatisha mahusiano yote na Israel.
Habari ID: 3481187 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/05
IQNA-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa onyo kali Alhamisi katika Makao Makuu ya Unmoja wa Mataifa jijini New York akilihimiza Baraza la Usalama na jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kuwalinda raia wa Gaza wanaokabiliwa na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3481151 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/29
IQNA- Maandamano yafanyika Uingereza kulaani mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel dhidi ya Gaza Maandamano makubwa yamefanyika nje ya ubalozi wa utawala wa Israel mjini London, Uingereza kulaani mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala huo dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3481127 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/24
IQNA – Katika Ukanda wa Gaza uliokumbwa na vita, dada watatu wa Kipalestina wamekamilisha kuhifadhi Qur’ani Tukufu yote, licha ya kuvumilia mashambulizi ya kijeshi ya Kizayuni, uhamisho wa kulazimishwa, na njaa kali.
Habari ID: 3481067 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/11
IQNA – Shirika la kutetea haki za Waislamu nchini Marekani limelaani vikali vifo vya raia wa Gaza vinavyosababishwa na njaa inayosababishwa kimakusudi na utawala wa Kizayuni wa Israel katika ukanda wa Palestina.
Habari ID: 3481043 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/06
IQNA – Kundi la walimu na maqarii mashuhuri wa Qur’ani kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeandika barua ya wazi kwa maqari wa Misri, likiwataka wachukue msimamo dhabiti dhidi ya ukatili wa utawala wa Kizayuni huko Gaza na kusimama pamoja na watu wanyonge wa eneo hilo.
Habari ID: 3481022 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/30
IQNA-Jeshi la majini la utawala ghasibu wa Israel limeiteka meli ya misaada iliyokuwa ikielekea Ukanda wa Gaza, ikiwa na bendera ya Uingereza, katika harakati za kuvunja mzingiro mkali wa eneo hilo unaoendelea tangu mwaka 2007.
Habari ID: 3481010 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/27
IQNA – Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Kiislamu kutoka Iran amewataka viongozi wa Kiislamu na Kiongozi wa Kanisa Katoliki kushikamana dhidi ya mzingiro wa Israel huko Gaza, ambako njaa inazidi kupelekea janga kubwa la kibinadamu.
Habari ID: 3480992 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/24
IQNA – Sheikh Ahmed al-Tayeb, Imamu Mkuu wa Al-Azhar, ametoaito wa dharura kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati mara moja kuokoa watu wa Gaza dhidi ya baa la njaa linalokatili maisha ya wengi.
Habari ID: 3480989 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/23
IQNA – Papa Leo XIV amelaani vikali vita vinavyoendelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel Gaza, akielezea vita hiyo kuwa ya “kinyama” na kukosoa matumizi holela ya nguvu, huku makumi ya Wapalestina wakiripotiwa kuuawa wakiwa kwenye foleni ya msaada wa chakula.
Habari ID: 3480975 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/21
IQNA – Msomaji wa Qur’ani wa Palestina na mwimbaji wa kaswida za Kiislamu amekufa shahidi katika shambulizi la hivi karibuni la anga lililofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3480954 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/16
IQNA – Kundi la watu wanaojiita viongozi wa Kiislamu na maimamu wa jamii za Waislamu barani Ulaya limekumbwa na ukosoaji mkali baada ya kufanya ziara katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu wiki hii, wakati ambapo utawala wa Kizayuni unaendelea na mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza.
Habari ID: 3480930 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/12
IQNA - Mgogoro mkubwa wa maji unatishia Wapalestina wa Gaza ambapo wanaweza kufariki kutokana na kiu cha maji huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo.
Habari ID: 3480860 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/26
IQNA - Jeshi katili la Israel dhid limeua takriban Wapalestina 56,077 katika mauaji ya kimbari huko Gaza tangu Oktoba 7, 2023.
Habari ID: 3480856 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/25
IQNA-Tume huru ya Umoja wa Mataifa imeutuhumu utawala wa Israel kwa kufanya mauaji ya halaiki kwa kuwashambulia raia wa Kipalestina wanaohifadhiwa katika shule na maeneo ya kidini huko Gaza.
Habari ID: 3480822 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/11
IQNA-Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa Linalowahudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) amezitaka nchi za Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi kutenga tone tu la fedha zilizotajwa katika ‘makubaliano makubwa’ kati yao na Rais wa Marekani, Donald Trump, ili kusaidia wakimbizi wa Kipalestina wanaopambana kuendelea kuishi katika ardhi zao ambazo Israel imezikalia kwa mabavu na pia wale wanaoishi katika nchi jirani.
Habari ID: 3480762 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/30
IQNA-Zaidi ya watu mashuhuri 300, wakiwemo waigizaji, wanamuziki na wanaharakati, wametuma barua kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, wakimtaka asitishe uungaji mkono wa Uingereza kwa Israel katika vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza.
Habari ID: 3480758 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/30
Spika wa Bunge la Iran katika Swala ya Ijumaa Indonesia
IQNA-Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge la Iran), Mohammad Baqer Qalibaf, ametoa wito kwa Waislamu kuimarisha umoja na kuwa sauti ya watu wa Palestina walioko Ukanda wa Gaza, ambao wanakumbwa na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Israel.
Habari ID: 3480692 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/16
IQNA – Mohsen Mahdawi, mwanafunzi wa Kipalestina katika Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani aliyekamatwa kwa kushiriki maandamano kupinga vita vya Israel dhidi ya Gaza, ameachiwa huru kutoka kizuizini.
Habari ID: 3480623 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/02