iqna

IQNA

Watetezi wa Palestina
IQNA-Maandamano makubwa yamefanyika mbele ya ubalozi wa Israel mjini Washington DC, Marekani kulaani vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478443    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/03

Jinai za Israel
IQNA-Viongozi wa dunia wameendelea kulaani kitendo cha wanajeshi wa Israel kuwaua Wapalestina 116 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 760 waliokuwa wakisubiri msaada wa chakula katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa siku ya Alhamisi.
Habari ID: 3478438    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/02

Jinai za Israel
IQNA - Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kusikitishwa kwake na ukatili ambao utawala wa Israel imekuwa ukitekelezwa kwa miezi kadhaa vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478435    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/03/01

Matukio yanayohusu Palestina
IQNA-Gazeti la New York Post limechapisha maelezo mapya kuhusu mwanajeshi wa Jeshi la Anga la Marekani, Aaron Bushnell ambaye alijichoma moto mbele ya ubalozi wa Israel mjini Washington akipinga mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo dhidi ya watu wa Gaza, na kumnukuu rafiki yake akisema kwamba Bushnell alimwambia ameona taarifa za siri zinazoonyesha ushiriki wa "vikosi vya jeshi Marekani katika kuua idadi kubwa ya Wapalestina.”
Habari ID: 3478433    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/29

Jinai za Israel
IQNA - Brazil imesisitiza haja ya utawala haramu wa Israel kufuata kikamilifu hatua za dharura zilizoamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) mwezi uliopita kuhusu hali ya Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478421    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/27

Jinai za Isarel
IQNA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesikitishwa na mauaji ya utawala haramu wa Israel dhidi ya raia katika Ukanda wa Gaza, akisema hali hiyo inatishia sheria za kimataifa za kibinadamu.
Habari ID: 3478420    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/27

Watetezi wa Palestina
IQNA-Waziri Kiongozi wa Scotland Humza Yousaf ameitaka Serikali ya Uingereza kusitisha uuzaji wa silaha kwa utawala wa Israel kutokana na utawala huo wa Kizayuni kuendeleza mauaji ya kimbari ya raia Wapalestina katika Ukanda Gaza.
Habari ID: 3478417    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/26

Jinai za Israel
IQNA-Rais Luiz Inácio Lula da Silva wa Brazil amesema kuwa, kinachofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza ni mauaji ya KIMBARI.
Habari ID: 3478407    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/24

Jinai za Israel
IQNA-Mkuu wa Kitengo cha Asia Magharibi katika Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema: Idadi ya raia na waandishi wa habari waliouawa huko Gaza haina mfano.
Habari ID: 3478363    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/16

Harakati za Qur'ani
IQNA - Makumi ya watoto huko Rafah, kusini mwa Gaza, ambao wamehitimu katika mafunzo ya
Habari ID: 3478360    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/16

Watetezi wa Palestina
IQNA - Hatua za kivita za utawala wa Israel huko Rafah "zinathibitisha" usahihi wa kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya utawala huo katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesema.
Habari ID: 3478356    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/15

Kadhi ya Palestina
IQNA-Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani mashambulizi yanayoendelea kufanywa na jeshi katili la Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza na upanuzi wa mashambulizi ya kiholela ya utawala huo kwenye mji wa Rafah, kusini mwa ukanda huo.
Habari ID: 3478355    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/15

Watetezi wa Palestina
IQNA-Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimelaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza, na kuonya kuhusu maafa ya binadamu katika eneo hilo.
Habari ID: 3478350    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/14

Jinai za Israel
IQNA-Utawala katili wa Israel umeendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza kwa kutekeleza mashambulizi makubwa ya anga na mizinga katika mji wa Rafah kusini mwa ukanda huo na kuua na kujeruhi mamia ya raia wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Habari ID: 3478339    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/12

Jinai za Israel
IQNA - Msichana wa Kipalestina mwenye umri wa miaka sita, ambaye alikuwa ametoweka kwa wiki mbili baada ya gari la familia yake kufyatuliwa risasi na wanajeshi katili wa utawala haramu wa Israel, alipatikana amekufa.
Habari ID: 3478327    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/10

Jinai za Israel
IQNA-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limeonya kwamba mashambulizi ya utawala haramu wa Israel dhidi ya mji wa mpakani wa Rafah wenye msongamano mkubwa wa watu Gaza yatakuwa "kichocheo cha maafa."
Habari ID: 3478326    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/09

Watetezi wa Palestina
IQNA - Siku ya pili ya Kimataifa ya Hatua kwa Ajili ya Gaza itaadhimishwa baadaye mwezi huu kwa maandamano ya mshikamano na watu wa Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3478312    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/06

Watetezi wa Palestina
IQNA - Watu katika nchi kadhaa za Ulaya walifanya maandamano siku ya Jumamosi kutoa sauti ya mshikamano na watu wa Palestina na kutoa wito wa kusitishwa mara moja kwa vita vya Israel dhidi ya Gaza.
Habari ID: 3478303    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/04

Mtazamo
IQNA- Ikiwa imepita miezi minne ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza, utawala huo umeshindwa kufikia lengo la kuangamiza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, na pia haujaweza kuvunja azma na irada ya wakazi wa eneo hilo. Hivyo ili kujaribu kufidia kufeli huko, Wazayuni wakishirikiana na baadhi ya waitifaki wao wa Magharibi, sasa wanalenga kusambaratisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA.
Habari ID: 3478288    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/01

Jinai za Israel
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema katika chapisho la ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X jana Jumapili kwamba kukata ufadhili kwa UNRWA "kutawaumiza tu watu wa Gaza".
Habari ID: 3478278    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/30