TEHRAN (IQNA) - Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameashiria ujumbe wa Twitter wa Rais Donald Trump wa Marekani ambaye ametoa pendekezo la kufanyika duru mpya ya mazungumzo ya nyuklia na Tehran na kusisitiza kuwa, mapambano ya Kiislamu au muqawama ndio njia pekee ya kumshinda adui.
Habari ID: 3472843 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/06
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kutumia kitabu cha Biblia kwa ajili ya kuhalalisha jinai na ukatili wa serikali yake na kuwahadaa Wamarekani.
Habari ID: 3472836 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/04
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Bahrain amesema Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyoongozwa na Imam Khomeini- Mwenyezi Mungu Amrehemu- yanafanana na ya Mitume- Mwenyezi Mungu Awarehemu- na kusisitiza kwamba umma wote wa Kiislamu una wajibu wa kuyalinda mapinduzi hayo.
Habari ID: 3472834 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/04
TEHRAN (IQNA) - Tarehe 14 Khordad sawa na tarehe 3 Juni, kulitangazwa habari ya huzini ya kuaga duniani Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3472831 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/03
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema yanayojiri siku hizi Marekani yameweka wazi ukweli uliokuwa umefichwa nchini humo kuongeza kuwa: "Wamarekani wamefedheheka duniani kutokana na mienendo yao."
Habari ID: 3472830 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/03
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, watawala wa Marekani ni watuhumiwa wa kuvunja haki za kimsingi kabisa za binadamu na inabidi wapandishwe kizimbani kwenye mahakama za kimataifa.
Habari ID: 3472829 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/06/02
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani hatua mpya zilizochukuliwa na Marekani za kuuwekea vikwazo ushirikiano wa kimataifa wa nyuklia baina ya Iran na pande nyingine na kusema kuwa kitendo hicho kinavunja waziwazi azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Habari ID: 3472821 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/31
TEHRAN (IQNA) – Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema misikiti yote nchini itafunguliwa kwa ajili ya swala zote.
Habari ID: 3472820 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/31
TEHRAN (IQNA) - Spika mpya wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran amesisitizia umuhimu wa umoja wa nchi za Kiislamu na jitihada za pamoja za kukabiliana na njama za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3472818 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/30
TEHRAN (IQNA) - Mohammad Bagher Qalibaf amechaguliwa kuwa spika mpya wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran. Kikao cha kumchagua spika wa bunge la 11 la Jamhuri ya Kiislamu kimefanyika Alhamisi asubuhi.
Habari ID: 3472810 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/28
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei ametuma salamu za pongezi katika sherehe za kuanza awamu ya 11 ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, na kusema kwa mara nyingine, demokrasia ya Kiislamu imeonyesha mvuto wake duniani.
Habari ID: 3472807 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/27
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuyapa mataifa ya Afrika uzoefu wake katika suala la kupambana na ugonjwa wa COVID-19 (Corona).
Habari ID: 3472802 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/26
TEHRAN (IQNA) - Wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo wameshiriki katika swala ya Idul Fitr baada ya kukamilisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3472797 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/24
Rais Hassan Rouhani wa Iran
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kukaribia maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kusisitiza kuwa, Quds (Jerusalem) katu haitasahauliwa na haitaendelea kubakia katika uvamizi wa madhalimu.
Habari ID: 3472785 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/20
Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Kamandi ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Intifadha ya taifa la Palestina imeshavuka mipaka ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kuingia kwenye awamu itakayoamua hatima yake na akasisitiza kwamba: Minong'ono ya kufikia tamati Israel ghasibu inasikika kwenye mitaa ya Tel Aviv.
Habari ID: 3472784 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/20
TEHRAN (IQNA) - Majlisi ya Ushauri ya Kiisalmu (Bunge la Iran) imeidhinisha muswada wa namna ambavyo Iran itakabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika upeo wa kitaifa na kimataifa.
Habari ID: 3472779 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/19
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Siku ya Kimataifa ya Quds itaadhimishwa nchini Iran na pia Swala ya Idul FItr itaswaliwa kwa kuzingatia kanuni za afya kuhusiana na ugonjwa wa COVID-19.
Habari ID: 3472770 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/16
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Mambo ya Nje Iran imetoa tamko kuhusu siku ya "Nakba" yaani siku ya nakama ya kuasisiwa utawala pandikizi wa Kizayuni katika ardhi walizoporwa Wapalestina na kusisitiza kuwa, kadhia ya Palestina itaendelea kuwa suala kuu nambari moja katika ulimwengu wa Kiislamu licha ya kufanyika njama nyingi za kulisahaulisha.
Habari ID: 3472767 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/15
TEHRAN (IQNA) - Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) imepasisha kwa kauli moja muswada wa dharura wa kukabiliana na njama na uhasama za utawala wa Kizayuni wa Israel, dhidi ya amani na usalama wa kieneo na kimataifa.
Habari ID: 3472759 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/12
TEHRAN (IQNA) – Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds ya mwaka huu yanatazamiwa kufanyika katika ukumbi wa Instagram na mitandao mingine ya kijamii nchini Afrika Kusini, kutokana na janga la corona.
Habari ID: 3472758 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/05/12