IQNA

Muqawama na Qur'ani

‘Qur'ani Tukufu imewawezesha watu wa Gaza kuwa na uvumilivu, umoja’

17:31 - August 10, 2024
Habari ID: 3479257
IQNA - Jumuiya ya Qur'ani ya Iran imesema subira na ustahimilivu wa watu wa Gaza dhidi ya uhasama wa Israel unatokana na mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

Gaza imekuwa nembo ya Uislamu kutokana na imani yake iliyokita mizizi katika Qur'ani Tukufu na kushikamana kwa uthabiti na mafundisho yake wakati wa matatizo, jumuiya hiyo ilitangaza katika taarifa yake siku ya Ijumaa.

"Qur'an imewapa watu wa Gaza subira, umoja, matumaini na bishara njema," iliongeza.

Taarifa hiyo ilisomwa katika hafla ya Khitma iliyofanyika mjini Ijumaa katika Ukumbi wa Swala (Mosalla) wa Imam Khomeini (RA) mjini Tehran baada ya Swala za Maghribi na Ishaa, kwa ajili ya shahidi Ismail Haniya, hayati kiongozi wa Hamas aliyeuawa katika shambulizi la Israel mwishoni mwa mwezi uliopita.

Taarifa hiyo ilianza kwa  kunukuu aya ya 171 na 172 za Surah As-Saffat, zinazosema: “Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa. Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa."

Halikadhalika Jumuiya ya Qur'ani ya Iran katika taarifa hiyo imelaani vikali mashambulizi ya kikatili ya Israel dhidi ya wanawake na watoto wa Kipalestina wasio na ulinzi, na kubainisha kwamba hujuma dhidi ya Gaza inaonyesha "sura mbaya" ya utawala wa Israel.

"Shahidi Ismail Haniya, shahidi wa Qur'ani, aliongoza kizazi kupitia mafundisho ya Qur'ani," ilisema taarifa hiyo.

Haniya aliwafedhehesha maadui na kueneza ujumbe wa Qur'ani unaoleta uhai na kujenga binadamu duniani, na kuzifanya aya zake tukufu zisikike tena, ilisema kauli hiyo, ikinukuu, aya ifuatayo ya Qur'ani: "Sema: Hivyo mnatutazamia litupate lolote isipo kuwa moja katika mema mawili? Na sisi tunakutazamieni kuwa Mwenyezi Mungu akufikishieni adhabu itokayo kwake, au kutokana na mikono yetu. Basi ngojeni, nasi tunangoja pamoja nanyi.” (Sura At-Tawba, aya ya 52).

" Kilichomtia hofu zaidi adui ni mwamko wa watu duniani kote, kuongezeka nguvu ya mapambano au muqawama, kuenea kwa mafunzo Qur’ani Tukufu na Uislamu, kuimarika kwa umoja wa Waislamu, na kushindwa kwa juhudi kubwa za adui za kuendeleza chuki ya Uislamu, migawanyiko na kutokuwa na dini. Maadui pia wameshindwa kuwaleta watu chini ya satwa yao,” imebaini taarifa hiyo.

3489433

Habari zinazohusiana
captcha