IQNA

Harakati za Qur'ani

Qari maarufu asisitiza usaidizi wa wazazi katika kukuza stadi za Qur’ani kwa watoto

21:25 - December 18, 2024
Habari ID: 3479918
IQNA – Qari wa ngazi za juu wa kike wa Qur’ani nchini Iran  amesema mazingira ya kuunga mkono na ya kutia moyo yanayotolewa na wazazi yana jukumu muhimu katika kukuza talanta za Qur’ani kwa watoto.

Zeinab Khazalizadeh, anayetoka Mkoa wa Khuzestan, alifanikiwa kushika nafasi ya tatu katika kitengo cha usomaji wa Qur'ani katika Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani kwa Wanawake nchini Iran. Katika mahojiano na IQNA, amesema mafanikio aliyoypata ni kwa hisani ya familia yake.

"Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa mafanikio niliyopewa; yote haya yanatokana na baraka za Qur’ani na Ahlul-Bayt (AS). Muhimu ni kuwa katika njia ya Qur’ani na kuifanyia kazi," amesema.

Akitafakari juu ya safari yake, Khazalizadeh alitaja kwamba wazazi wake wameunganishwa kwa kina na Qur’ani, na mama yake akihudumu kama mwalimu wa Kurani.

Alianza kuhifadhi Qur'ani katika miaka yake ya msingi na, baada ya kutambua kipaji chake cha kusoma, alianza mafunzo maalum akiwa na umri wa miaka 12, akipokea mwongozo kutoka kwa walimu mbalimbali.

Anaiga mtindo wa bwana wa Kimisri Mustafa Ismail na hivi karibuni alipata cheo cha msomaji wa shahada ya pili kutoka kwa Baraza Kuu la Qur'ani, heshima kubwa nchini Iran.

Khazalizadeh aliashiria umuhimu wa mazingira ya kusaidia katika kukuza vipaji vya mtoto vya Qur'ani, na kuwashauri wazazi kuwezesha fursa bila ya kuweka shughuli maalum.

Alibainisha kuwa watoto wanapowaona wazazi wao wakifanya mazoea kama vile swala kwa kawaida wana mwelekeo wa kufuata mfano huo.

Akizungumzia jinsi familia za Qur'ani zinavyoweza kukabiliana na changamoto za kijamii, Khazalizadeh alitoa mfano wa mafundisho ya Qur'ani ambayo yanasisitiza subira na swala.

Alionya kwamba kuonekana kuwa mtu wa kidini tu hakutoshi kwa kupinga vishawishi na magumu; kuelewa na kujumuisha aya za Qur’ani huwawezesha watu binafsi kustahimili hali ngumu zaidi za maisha.

Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran, yaliyoandaliwa na Shirika la Masuala ya Wakfu na Misaada, yalihitimisha sehemu zake za wanawake na wasichana walio chini ya umri wa miaka 18 kwa sherehe huko Tabriz, tarehe 9 Disemba 2024, baada ya wiki ya mashindano.

Tukio hilo liliwaonyesha wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani wakuu wa taifa , likilenga kukuza maadili ya Kiislamu na kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika wa Qur'ani.

Sehemu ya wanaume ya mashindano hayo inafanyika Tabriz kuanzia Desemba 10-19.

4253831

Habari zinazohusiana
captcha