IQNA

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani kwa Wanafunzi wa Al-Azhar wazawadiwa

16:22 - April 22, 2025
Habari ID: 3480582
IQNA – Washindi wa mashindano ya kimataifa ya kukumbuka Qur’ani kwa wanafunzi wa kigeni wa Al-Azhar wametunukiwa zawadi katika sherehe iliyofanyika nchini Misri mwishoni mwa wiki. Shirika la Kimataifa la Wahitimu wa Al-Azhar lilipanga sherehe hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Hisani ya Abu Al-Ainain.

Zaidi ya wanafunzi elfu moja wa kiume na kike wa Al-Azhar kutoka mataifa mbalimbali waliosoma katika taasisi hii ya Kiislamu walishiriki katika mashindano hayo.

Sheikh Abbas Shoman, mwenyekiti wa baraza la utawala la shirika hilo, Somaya Abu Al-Ainain, makamu wa rais wa taasisi hiyo ya hisani, Nahla Saeedi, mshauri wa Sheikh wa Al-Azhar kuhusu masuala ya wanafunzi wa kigeni, na maafisa wengine kadhaa kutoka Shirika la Kimataifa la Wahitimu wa Al-Azhar walihudhuria sherehe hiyo. Katika hotuba yake katika tukio hilo, Sheikh Shoman alisema Qur’ani Tukufu ni nuru ambayo vijana wanastahili kuitumia ili kupata mwongozo na mafanikio katika dunia iliyojaa vurugu na machafuko. 

Aliongeza pia kushukuru kwake kwa juhudi za taasisi hiyo katika kusaidia wahifadhi wa Qur’ani na kuwahimiza kukumbuka, kusoma, na kuelewa Neno la Allah. Aidha amebaini  kuwa Al-Azhar inashirikiana na mashirika mengi ya hisani, ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Hisani ya Abu Al-Ainain, na ina uwepo wa kawaida katika shughuli za hisani na programu za Qur’ani.

 Mashindano ya kimataifa ya kukumbuka Qur’ani kwa wanafunzi wa kigeni wa Al-Azhar yaliandaliwa katika kategoria za kuhifadhi Qur’ani kikamilifu, kuhifadhi nusu ya Qur’ani na sauti nzuri zaidi. Mwisho wa mashindano, watu 35 walitambuliwa kama washindi wa juu na kukabidhiwa zawadi zao.

3492791

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu al azhar
captcha