
Msahafu huu una vipimo vya sentimita 312 kwa 220, na una kurasa 700, jambo lililopelekea makumbusho hayo kutambuliwa rasmi na Shirika la Rekodi Duniani, Guinness, kwa kuonyesha Qur’ani kubwa zaidi duniani, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Saudi (SPA).
Kwa mujibu wa SPA, maandiko hayo ni toleo lililopanuliwa (magnified reproduction) la Qur’ani ya kihistoria inayorejea karne ya 16 Miladia.
Nakala ya asili ina vipimo vya sentimita 45 kwa 30, ambapo sura nyingi zimeandikwa kwa hati ya Thuluth, huku Surat al-Fātiḥa ikiandikwa kwa hati ya Naskh. Mpangilio huu unaakisi ladha ya hali ya juu ya kisanaa pamoja na utofauti wa mitindo ya kaligrafia uliokuwapo katika zama hizo.
Nakala hii ya Qur’ani ni mfano wa kipekee wa sanaa ya uandishi wa Kiarabu, upambaji wa dhahabu (tadhhīb) na ufundi wa ufungaji wa vitabu. Inaonesha uzuri wa sanaa za Kiislamu kupitia mapambo ya kina, michoro ya umbo la jua katika ukurasa wa mwanzo, pamoja na kurasa za mwanzo na vichwa vya sura vilivyosanifiwa kwa ustadi mkubwa, vinavyoashiria kiwango cha juu cha umahiri wa kisanaa.

Msahafu huu uliwekwa wakfu mwaka 1883. Nakala yake ya asili kwa sasa imehifadhiwa katika Jumba la Mfalme Abdulaziz la Maktaba za Wakfu, na unasalia kuwa ushahidi wa kudumu wa heshima kuu waliyonayo Waislamu kwa Qur’ani Tukufu, pamoja na utajiri na kina cha sanaa za Kiislamu katika mfululizo wa karne nyingi.
3496305