IQNA

Jumuiya ya Qur'ani ya Iran inafungamana na utamaduni wa kupinga utawala wa Kizayuni

20:32 - June 15, 2025
Habari ID: 3480838
IQNA – Naibu Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu Iran ambaye anasimamia masuala ya Qur'ani na Itrah amelaani vitendo vya hivi karibuni vya uchokozi vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran na kusisitiza azma ya jumuiya ya Qur'ani nchini kufungamana na utamaduni wa muqawama (mapambano ya Kiislamu) na kuupinga utawala wa Kizayuni sambamba na kutetea maadili ya Kiislamu.

Hujjat-ul-Islam Hamid Reza Arbab Soleimani ametoa ujumbe Jumamosi, akilaani mashambulizi ya utawala wa Israeli yaliyosababisha kuuawa shahidi kwa makamanda kadhaa wa kijeshi wa Iran, wanasayansi na raia.

Alisisitiza kuendelea kwa njia ya Muqawama na utetezi wa maadili ya Kiislamu, amewataka watumishi wa Qur'ani kote nchini kupaza sauti ya uthabiti, imani, na matumaini kwa lugha ya Qur'ani.

Huu hapa ujumbe wake kamili:

"Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

'Walio amini wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio kufuru wanapiana katika njia ya upotofu. Basi piganeni na marafiki wa Shet´ani. Hakika hila za Shet´ani ni dhaifu.' (Aya ya 76 ya Sura An-Nisaa)

Enyi taifa kubwa na tukufu la Iran! Kufuatia uchokozi wa waziwazi wa utawala dhalimu na mhalifu wa Kizayuni dhidi ya ardhi iliyotakasika ya Iran ya Kiislamu na kuuawa shahidi kwa makamanda kadhaa, wanasayansi, wasomi, na raia wasio na hatia, sisi, watumishi wa Qur'ani Tukufu kote nchini, tukitegemea mafundisho ya milele ya Wahyi wa Mwenyezi Mungu, kwa utiifu kamili kwa matakwa ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei, na kuendeleza njia tukufu ya mashahidi wenye fahari wa ardhi hii, huku tukilaani vikali uhalifu huu, mara nyingine tena tunatangaza upya ahadi yetu na utamaduni wa Muqawama, kutafuta heshima, na kutetea utukufu wa Ummah wa Kiislamu na utakatifu wa Qur'ani na Ahlul-Bayt (AS).

Shambulio hili la uoga si ishara ya nguvu ya adui bali ni dalili wazi ya kukata tamaa na hofu yao mbele ya kuamka kwa safu ya haki dhidi ya batili. Kwa maana (kama Qur'ani inavyosema,)

"Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu. ' (Aya ya 160 ya Sura Al-Imran)

Jumuiya ya Qur'ani ya Iran, ikiongozwa na damu safi ya mashahidi na kuamini ahadi zisizoshindwa za Mwenyezi Mungu, ina uhakika kwamba desturi ya Mwenyezi Mungu ya kuwaunga mkono wanyonge na kuwaangamiza madhalimu ni kamili na ya kudumu. Adui ajue: Taifa ambalo nyoyo zake zimetolewa kwa Qur'ani na njia yake imeangazwa na urithi wa Imam Hussein (AS) haliogopi vitisho wala halirudi nyuma mbele ya dhuluma.

"Basi msiregee na kutaka suluhu, maana nyinyi ndio mtakao shinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu..' (Aya ya 35 ya Sura Muhammad)

Idara ya Qur'ani na Itrah inawaalika watumishi wote wa Qur'ani, wasomaji, wahifadhi, wanazuoni, wanaharakati, na taasisi za Qur'ani kote nchini, katika nyakati hizi za maamuzi, kukuza kilio cha uthabiti, imani, na matumaini katika ushindi wa haki juu ya batili, katika vikao vya ana kwa ana na mitandanoni, ,kupitia lugha ya Qur'ani.

'…Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.' (Aya ya 40 ya Sura Al-Hajj)

Aidha tunatangaza kuwa: Qur'ani ni bendera ya heshima yetu, na imani ni silaha isiyoshindika ya taifa letu. Ikiwa adui alikuja kututikisa nyoyo zetu, sasa ajue kwamba mwako wa imani umefanya vifua vyetu kuwaka zaidi na safu zetu kuungana zaidi. Tukiongozwa na damu ya mashahidi na kwa ufahamu na utiifu kwa Wali Faqih (Faqihi Mtawala) wa zama zetu, tutasimama imara hadi kutimia kwa ahadi ya uhakika ya Mwenyezi Mungu, wala hatutateteleka. Hatuna shaka kwamba ushindi umekaribia. Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi.' (Aya ya 5 ya Sura Al-Qasas)"

3493439

 

captcha