IQNA

Ayatullah Sistani alaani mashambulizi ya kikatili ya Israel dhidi ya Iran

19:34 - June 13, 2025
Habari ID: 3480830
IQNA-Kiongozi Mkuu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq amelaani vikali uchokozi wa hivi karibuni wa utawala wa Israel dhidi ya Iran, na ameihimiza jamii ya kimataifa kuzuia mashine ya vita ya utawala huo wa Kizayuni.

"Kitendo cha uhalifu kilichofanywa na utawala wa Kizayuni unaokalia kwa mabavu ardhi za katika saa za mapema za Ijumaa, kilichosababisha kuuawa kwa mashujaa kadhaa wa Iran, ikiwa ni pamoja na wanasayansi, makamanda wa kijeshi, na raia wa kawaida, wakiwemo wanawake na watoto, pamoja na mashambulizi dhidi ya taasisi kadhaa za elimu na sayansi, kwa mara nyingine kinadhihirisha tabia ya uchokozi na hatari ya utawala huu," Ayatullah Seyyed Ali Sistani aliandika katika taarifa ya Ijumaa.

"Tunawaombea rehema na daraja za juu mashujaa waliouawa, tunatoa rambirambi kwa familia zao, na tunawatakia ahueni ya haraka waliojeruhiwa na walioathirika. Tunalaani vikali kitendo hiki cha kikatili," alisema.

"Tunatoa wito kwa jamii ya kimataifa kushinikiza utawala huu wa uchokozi na wafuasi wake ili kuzuia vitendo zaidi vya uvamizi," aliongeza.

Taarifa hii inakuja baada ya Israel kufanya mashambulizi katika majimbo kadhaa ya Iran, ikiwemo mji mkuu, Tehran. Milipuko imeripotiwa katika miji mbalimbali, huku video na picha kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha uharibifu mkubwa na huduma za dharura zikijibu matukio hayo.

Miongoni mwa waliouawa shahidi katika mashambulizi hayo ni maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi wa Iran, akiwemo Meja Jenerali Mohammad Bagheri, Mkuu wa Majeshi ya Iran, na Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). Ripoti pia zinaonyesha kuwa vituo vya kijeshi na vya nyuklia, ikiwemo kituo cha nyuklia cha Natanz, vililengwa katika mashambulizi hayo.

 

3493433

Habari zinazohusiana
captcha