IQNA

Wanachama wa Msafara wa Qur'ani wa Iran kwa ajili ya Hija 1447 Watajwa

10:08 - February 09, 2026
Habari ID: 3481906
IQNA – Majina ya wanachama wa Msafara wa Qur'ani wa Nurwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, unaotarajiwa kuelekea Ufalme wa Saudi Arabia wakati wa msimu wa Hija mwaka huu, yametangazwa rasmi.

Msafara huo utasimamia na kuendesha programu mbalimbali za Qur'ani Tukufu katika kipindi cha ibada hiyo tukufu. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, msafara huo unajumuisha qurra na mahafidh 14 wa Qur'ani Tukufu, pamoja na kikundi cha Tawasheeh chenye wanachama watano. 
Wateule hao walipatikana baada ya kufanyiwa mitihani ya ushindani na tathmini za kitaalamu.
Majina ya qari na mahafidh walioteuliwa ni: Hamed Shakernejad kutoka Khorasan Razavi, Mehdi Shayeq wa Yazd, Mokhtar Dehghan wa Khorasan Razavi, Seyed Sadeq Moslemi wa Mazandaran, Ali Hezbian wa Khuzestan, Sajjad Ansaripour wa Khorasan Razavi, Vahid Karami wa Lorestan, Saeed Jabbari wa Azerbaijan ya Mashariki, Seyed Mohammad Hossein Zakeri wa Azerbaijan ya Magharibi, Davud Karimi wa Tehran, Mohammad Esmaili wa Ardabil, Masoud Safari wa Hamedan, Meysam Sarwarifar wa Qazvin, na Mohammad Khakpour wa Khorasan Razavi.
 
Aidha, kikundi cha Tawasheeh cha Habl al-Matien kutoka Mkoa wa Zanjan kitaandamana na msafara huo. Wanachama wa kikundi hicho ni Saeed Amanloo, Mohammad Javad Rezaei, Mehdi Karami, Saeed Doyran, na Ali Qanbari. Uongozi wa Msafara wa Qur'ani wa Nur utakuwa chini ya Seyed Mee’ad Salehi kutoka Tehran. 
 
Habari inayohusiana:
Kila mwaka, mamilioni ya Waislamu kutoka pembe zote za dunia hukusanyika katika Mji Mtukufu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija. Iran, sambamba na kuwatuma mahujaji wake, pia hupeleka ujumbe maalumu wa wanazuoni na wahudumu wa Qurani, wanaojulikana kama Msafara wa Qur'ani wa Nur. Wanachama wa msafara huu huendesha shughuli mbalimbali za Qur'ani, zikiwemo vijiwe vya qiraa na vikao vya kisomo cha Qur;ani, kwa ajili ya mahujaji katika miji mitukufu ya Makka na Madina. 
Msafara wa Qur'ani wa Nur ni sehemu ya juhudi pana za Iran katika kuimarisha tajriba ya kiroho ya mahujaji wake, kwa kuratibu na kuhuisha programu za Qur'ani wakati wa msimu wa Hija,ibada inayobeba umoja, unyenyekevu na nuru ya Uislamu kwa Umma mzima.

3496340/

captcha