IQNA

Vita dhidi ya Iran havikidhi vigezo vya “Vita vya Haki”, asema Papa Leo

15:54 - June 07, 2026
Habari ID: 3482334
IQNA – Katika kauli yenye ukali dhidi ya sera za Rais wa Marekani Donald Trump, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amesema kwamba vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran havina uhalali wa maadili.

Papa Leo wa Kumi na Nne amesema kuwa vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran havitimizi viwango vya “vita vya haki” kwa mujibu wa mafundisho ya Katoliki, akirudia msimamo aliowahi kutoa hapo awali wakati wa ziara yake mjini Madrid.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari akiwa safaraini kutoka Roma, Italia kuelekea Madrid, Hispania Kiongozi wa Kanisa Katoliki alisema: “Katika suala la Iran, vigezo vya kuhalalisha vita vya haki havipo.”

Ameongeza kuwa nadharia ya jadi ya vita vya haki iliundwa katika kipindi ambacho binadamu hangeweza kufikiria kiwango cha uharibifu wa silaha za kisasa.

Kauli hizi zinakuja baada ya tofauti za awali na Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance, ambaye alikuwa ametetea mzozo huo kama “vita vya haki”, jambo ambalo Papa alilikataa.

3497744

Habari zinazohusiana
Kishikizo: papa iran vita marekani
captcha