IQNA

Kiongozi wa Kanisa Katoliki akosoa vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, avitaja kuwa aibu kwa ubinadamu

15:48 - March 23, 2026
Habari ID: 3482082
IQNA – Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo amekosoa vikali vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, akivitaja kuwa ni fedheha kwa familia nzima ya kibinadamu na mtihani mkubwa wa maadili kwa ulimwengu mzima.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki alitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano kutokana na idadi kubwa ya wananchi wasiokuwa na hatia wanaoathirika.

Ametoa matamshi hayo wakati wa sala ya kila wiki ya Angelus katika Uwanja wa Mtakatifu Petro huko Vatican Kwa mujibu wa Papa Leo, dunia haina haki ya kubaki katika hali ya kutojali mateso ya raia.

“Hatuwezi kukaa kimya mbele ya mateso ya watu wengi, wahanga wasio na ulinzi wa mizozo hii. Kinachowaumiza wao, kinaumiza ubinadamu wote,” alisisitiza.

Papa Leo amesema kuwa matukio yanayoendelea Mashariki ya Kati yanamletea wasiwasi mkubwa.

Ameeleza kuwa anaendelea kufuatilia kwa tahadhari yanayojiri si tu katika eneo hilo, bali pia katika maeneo mengine ya dunia ambako vita na vurugu bado vinaendelea. Kilicho muhimu zaidi, kwa mujibu wake, ni kwamba mgogoro huo umekuwa wa muda mrefu na unaendelea kwa wiki kadhaa.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katololiki amesisitiza tena mwito wake kwa jamii ya kimataifa kusitisha uhasama na kufungua njia ya suluhu ya amani.

“Naendelea kusisitiza kwa nguvu zote umuhimu wa kuomba kwa udumu ili mapigano yakome, na njia ya amani ifunguliwe hatimaye.”

3496854

captcha