IQNA

Hatua ya Awali ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Iran kuanza mwezi ujao

11:53 - June 09, 2026
Habari ID: 3482343
IQNA – Zaidi ya watu 67,000 wamejiandikisha kushiriki katika Mashindano ya 49 ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambapo hatua ya awali inatarajiwa kuanza mwezi ujao.

Muda wa mwisho wa kujiandikisha, ambao ulikuwa umeongezwa mara moja, ulikamilika mwishoni mwa mwezi Mei.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, jumla ya washiriki 67,843 watashiriki katika vipengele mbalimbali vya mashindano. Mikoa ya Khorasan Razavi na Isfahan imeongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya waliojisajili.

Kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa, hatua za wilaya na mkoa zitaanza mwezi ujao. Washiriki watakaofanya vizuri zaidi watafuzu kuingia hatua ya mwisho (fainali), ambayo imepangwa kufanyika mwezi Novemba katika mji wa Zahedan, mkoa wa kusini-mashariki wa Sistan na Balouchestan.

Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, huandaliwa na Shirika la Wakfu na Masuala ya Hisani, na ni mashindano makubwa zaidi ya Qur’ani nchini, Mashindano hayo ya kila mwaka yanambuliwa kama tukio lenye hadhi ya juu zaidi ya Qur’ani nchini Iran, na hulenga kuendeleza maadili ya Kiislamu, kukuza uelewa na umahiri wa Qur’ani, pamoja na kuenzi vipaji bora vya wanazuoni na wasomaji.

Hufanyika katika vipengele mbalimbali vikiwemo usomaji wa Qur’ani (Tilawah), Tarteel, hifdh (uhifadhi wa Qur’ani), na pia Adhana.

Washindi wa juu watapata heshima ya kuiwakilisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yanayofanyika katika nchi mbalimbali duniani.

3497773

captcha