IQNA

Waislamu Australia

Washindi wa Shindano la Qur'ani la Sydney 

22:43 - September 22, 2023
Habari ID: 3477636
CANBERRA (IQNA) - Mashindano ya Qur'ani yaliyoandaliwa mjini Sydney, Australia, yalihitimishwa katika sherehe ambapo washindi wa kwanza walitunukiwa.

Mashindano hayo yaliandaliwa na Samen Al-Aeme Imam Reza Quran Academy mnamo Septemba 15-17.
Washiriki kutoka sehemu mbalimbali za Australia pamoja na New Zealand walishindana kwa ajili ya tuzo za juu ya kusoma Qur'ani Tukufu.
Muhammad Taqi Saadi alikuja wa kwanza katika kategoria ya qiraa huku Muhammad Ali Saadi akinyakua tuzo ya juu katika Tarteel.
Katika kitengo cha Tarteel kwa wanawake, mshindi  mkuu alikuwa Larayb Malik mwenye asili yaPakistan.
Jopo la waamuzi lilijumuisha idadi ya wataalamu wa Qur'ani kama vile Habibullah Razban, Sheikh Mahdi al-Kana'ani na Hujat-ul-Islam Hussein Jawaheri.
Jopo hilo liliongozwa na Mustafa Ashrafi, ambaye pia ni rais wa Samen Al-Aeme Imam Reza Quran Academy.
Kwa mujibu wa Ashrafi, washindi hao wataiwakilisha Australia katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.
Chuo hicho kilianzishwa rasmi mwaka 2021 na huwakaribisha waumini 150 na 300 kwa ajili ya programu kama vile dua ya tawassul, Ashrafi aliiambia IQNA katika mahojiano.
Zaidi ya hayo, kituo hicho kila mwaka huandaa programu maalum za Qur'ani wakati wa Mwezi Mtukufu Ramadhani ambazo "zimekuwa na mafanikio makubwa," Ashrafi alisema.

 

4169767

Habari zinazohusiana
captcha