Bi.Azarman Sadeghi, ambaye alipata nafasi ya kwanza katika hafla ya kitaifa wiki iliyopita, amezungumza na shirika la habari la IQNA kuhusu jitihada zake.
Sadeghi, ambaye alianza kusoma Qur’ani akiwa na umri wa miaka sita anasema, "Sauti ya usomaji wa Qur'ani ilikuwepo kila mara nyumbani kwetu. Wazazi wangu walisoma Qur’ani, mama yangu aliunga mkono usomaji wetu, na baba alitununulia zawadi. Dada yangu ni pia ni mhifadhi wa Qur'an yote, na Alhamdulillah sisi ni familia ya Qur'ani."
Sadeghi, ambaye alishiriki katika mashindano hayo akiwa na mtoto wake mchanga, alijitolea ushindi wake kwa mama yake, ambaye alikuwa akingojea kwa hamu matokeo haya. "Nambusu mkono kwa sababu baada ya kifo cha baba yangu, amekuwa mama na baba kwetu," amesema.
Sadeghi alipoulizwa kuhusu changamoto za kushiriki mashindano hayo ya kitaifa akiwa na mtoto mdogo alijibu, "Haikuwa shida kwangu. Baraka mojawapo iliyonileta kwenye mashindano ya Qur'ani ni watoto wangu, ninapofanya mazoezi, watoto wangu husoma pamoja nami na mtoto wangu wa miaka saba anaiga mtindo wa msomaji mashuhuri wa Kimisri, Mustafa Ismail, na hata anasoma vizuri kuliko mimi.
"Mtoto wangu mdogo pia ana kipawa cha kukariri ninaposoma," alisema na kuongeza, "Kila kitu tulicho nacho kinatokana na baraka za Qur’ani. Mume wangu pia ni hafidh wa Qur'ani nzima."
Sadeghi ameangazia athari za Qur’ani katika maisha ya familia yake, akisema, "Katika misukosuko yote ya maisha, mimi na mume wangu tunamtegemea Mwenyezi Mungu, na hii ndiyo siri ya mafanikio yetu. Wasiwasi wetu mkubwa ni kulea watoto wa Qur’ani. Sisi hufanya mazoezi ya kusoma Qur’ani kama familia ambapo pia huwa tunachambua tafsiri ya kila neno na husikiliza pia qiraa ya maqari mashuhuri. Kuwa na Qur’ani juu ya meza nyumbani huleta utulivu maalum kwetu."
Hatua ya mwisho ya Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani kwa wanaume, yaliyoandaliwa na Shirika la Wakfu na Masuala ya Misaada, hivi sasa inafanyika Tabriz. Kitengo cha wanawake kilifanyika katika ukumbi huo kutoka Desemba 2 hadi 9 na sasa kategoria ya wanaume ingali inaendelea.
4253861