IQNA

Muswada Adimu wa Msahafu wa Karne ya 19 Waonyeshwa katika Makumbusho ya Makka

15:40 - April 21, 2026
Habari ID: 3482156
IQNA – Msahafu au nakala ya Qur’ani, iliyondikwa kwa mkono nchini India katika karne ya 19, imepelekwa kwenye maonyesho ya Makumbusho ya Qur’ani Tukufu katika eneo la utamaduni la Hira katika mji mtakatifu wa Makka.

Nakala hii adimu ya Qur'ani imetayarishwa  kwa umbo la kipekee la nane, ukitoa urahisi wa kubeba pamoja na upekee wa sanaa na ubunifu wa kaligrafia.

Maonyesho haya yanaunga mkono dhamira ya makumbusho ya kuwaelimisha wageni kuhusu historia na maendeleo ya kaligrafia ya Qur’ani, huku yakiongeza mvuto wa kiutamaduni na kitalii wa eneo hilo, na kutia nguvu nafasi ya Mecca katika ulingo wa kimataifa.

Makumbusho pia yanaonyesha nakala ya mlango wa Kaaba Tukufu, ikionyesha muunganiko wa uzuri wa sanaa na maana ya kiroho katika ustaarabu wa Kiislamu.

Nakala hiyo imepambwa kwa aya za Qur’ani zilizoandikwa kwa kaligrafia ya Kiarabu na mapambo ya Kiislamu yenye ustadi wa kipekee.

Mlango wa asili wa Kaaba ulitengenezwa wakati wa utawala wa Mfalme Khalid bin Abdulaziz, ukiwa na maelezo yaliyopambwa vizuri, yakiwemo aya za Qur’ani zikionesha utakatifu wa Kaaba.

Aya zilizochorwa zimepangwa kwa mpangilio maridadi, zikionesha ubunifu wa juu, ufundi bora, na mapambo ya mimea na ya kijiometri yanayozunguka.

Makumbusho pia lina mozaiki adimu inayoonyesha aya za mwanzo za Qur’ani Tukufu, kazi hii ikichanganya kaligrafia ya Kiarabu ya kuvutia na urithi wa sanaa za mapambo za Kiislamu.

Mozaiki hii ya karne ya 17 inaonesha ubora mkubwa wa ufundi na desturi ndefu ya kuelezea Qur’ani kwa njia za sanaa tofauti.

Makumbusho linaendelea kuvutia idadi kubwa ya wageni kupitia elimu na maonyesho bunifu, likimarisha nafasi ya Mecca kama kitovu cha utamaduni wa Kiislamu.

Eneo la utamaduni la Hira limejengwa jirani na Jabal Hira, mahali alikopokea Wahyi Mtume Muhammad (SAW) ndani ya pango la Hira, likipewa umuhimu mkubwa wa dini na historia.

Eneo hili linajumuisha miundombinu kadhaa muhimu, ikiwemo Makumbusho ya Qur’ani Tukufu, likielezea historia ya ukusanyaji na maendeleo ya Qur’ani, pamoja na maonyesho ya mwingiliano kuhusu kaligrafia ya Kiarabu na sanaa za Kiislamu.

3497167

Habari zinazohusiana
captcha