Maonesho hayo yameandaliwa na Urais wa Masuala ya Kidini wa Msikiti Mtukufu na Msikiti wa Mtume (SAW).
Maonesho hayo yanajumuisha nakala ya kipekee ya Qur’ani Tukufu iliyoandikwa na mwandishi wa hati mashuhuri, Ali bin Hilal, anayefahamika kama Ibn Al-Bawwab, zaidi ya miaka 1,000 iliyopita.
Msahafu huo nimoja ya vielelezo muhimu zaidi vya maonesho hayo, ikidhihirisha jinsi Waislamu walivyojali na kuhifadhi Qur’ani Tukufu katika zama zote.
Msahafu huo unaonyeshwa pamoja na faharasa ya kisayansi na uchambuzi wa usanii wa maandishi (khat) na mapambo yaliyopamba kurasa zake, jambo linalowaruhusu wageni kuchunguza thamani yake ya kihistoria na kisanaa, na kufuatilia maendeleo ya maandishi ya Kiarabu na mapambo ya Kiislamu katika karne nyingi zilizopita.
Hati hii inachukuliwa kuwa mojawapo ya hati adimu zaidi za Kiislamu kutokana na thamani yake kubwa ya kisayansi, kisanaa, na kihistoria.
Msahafu huu ni wa kipekee jambo linaloakisi hadhi ya juu ambayo Qur’ani Tukufu imekuwa nayo katika historia yote ya Kiislamu.
3498286