IQNA

Makumbusho ya Makka yanawasilisha historia ya kuhifadhiwa kwa Qur’ani

17:23 - July 14, 2026
Habari ID: 3482486
IQNA – Makumbusho mapya katika Eneo la Kitamaduni la Hira jijini Makka yanawazamisha wageni katika bahari ya historia ya uandishi wa Qur’ani Tukufu.

Makumbusho ya Qur’ani Tukufu yaliyopo katika Eneo la Kitamaduni la Hira jijini Makka, yanaonesha mifano halisi ya zana na vifaa vilivyotumika kuandikia Qur’ani Tukufu wakati wa zama za Mtume Muhammad (SAW).

Makumbusho hayo yanawapa wageni uzoefu wa kielimu unaochunguza chimbuko la uandishi wa Wahyi (ufunuo) na mbinu walizotumia Masahaba wa Mtume Muhammad (SAW) kunakili aya za Qur’ani.

Vitu vilivyowekwa maoneshoni ni pamoja na ngozi zilizosindikwa (parchments), makuti ya mitende, vipande vya mbao na mawe, pamoja na mifupa ya wanyama kama vile mifupa ya mabega na mbavu.

Vifaa hivi vilitumika kabla ya Qur’ani kukusanywa na kuwa kitabu KImoja (Msahafu). Maonesho hayo yanaambatana na maelezo ya kina na mawasilisho ya kisasa ya kidijitali yanayofafanua jinsi vifaa hivyo vilivyotumika, huku yakisisitiza juhudi kubwa zilizofanywa katika kuilinda na kuihifadhi Qur’ani katika umbo lake asilia.

Kama moja ya vivutio vikuu katika Eneo la Kitamaduni la Hira, makumbusho haya yanachimbua historia ya Qur’ani, sayansi zake, na hatua mbalimbali za uandishi na ukusanyaji kupitia kumbi za kisasa za maonesho na teknolojia shirikishi. Makumbusho haya yanawapa wageni fursa ya kujifunza kwa njia inayovutia na yenye mguso wa kipekee.

3498243

Habari zinazohusiana
captcha