IQNA

Ghadhabu baada ya Mzayuni kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu Al‑Quds, mkesha wa kuingia Ramadhani

11:12 - February 18, 2026
Habari ID: 3481955
IQNA — Video iliyosambaa siku ya Jumanne inaonyesha mlowezi Mzayuni akichoma nakala ya Qur’ani Tukufu katika mji wa al‑Quds (Jerusalem), kitendo cha makusudi cha kudharau kitabu kitakatifu cha Waislamu ambacho kinahatarisha kuchochea mvutano mkubwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Zayuni mwenye misimamo mikali yakdini kutoka kundi lenye mwelekeo wa Wanazi mamboleo amechoma Qur’ani Tukufu hadharani, bila kuficha uso wake,” alisema mbunge wa Kiarabu katika Bunge la Israel (Knesset), Ahmad Tibi, kupitia mtandao wa kijamii wa X .

Tibi amelalamika kuwa mlowezi huyo mwenye misimamo mikali “hataadhibiwa kwa sababu yeye ni Myahudi.”

Katika video aliyoshiriki Tibi, mlowezi huyo haramu wa Kizayuni anasikika akisema: “Kuna nini kinaendelea? Tuko hapa sasa tunasherehekea na kuchoma kitabu kitakatifu sana kwa Waislamu, sura kwa sura, sura zote. Hongera kwetu.”

Aliendelea kusema: “Watu wa Israel wanaondoa uovu. Hongera kwetu. Ninaiheshimu sana Qur’ani, lakini pale inapokuwa katika hali hii,” huku akiendelea kuchoma Kitabu Kitakatifu.

Hakukuwa na kauli ya haraka kutoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel wala kutoka kwa makundi ya Kiyahudi kuhusu tukio hilo, wakati huu Waislamu duniani kote wakianza kuukaribisha na kuadhimisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

3496456

Habari zinazohusiana
captcha