IQNA

Arbaeen 1446

Profesa wa Iraqi:  Matembezi ya Arbaeen ni bishara ya  Ustaarabu Mpya wa Kiislamu

23:22 - August 26, 2024
Habari ID: 3479330
IQNA - Matembezi ya Arbaeen ambayo huvutia mamilioni ya wafanyaziara kila mwaka ni ishara ya utambuzi wa ustaarabu mpya wa Kiislamu, mwanazuoni wa Iraq alisema.

Akizungumza na IQNA, Sattar Qassim Abdullah, ambaye anafundisha katika Chuo Kikuu cha Dhi Qar, aliangazia vipengele tofauti vya kidini, kijamii, kisiasa na kiroho vya ibada ya matembezi ya Arbaeen.

Ameitaja ibada matembezi ya Arbaeen kuwa kubwa zaidi ya aina yake duniani hivi sasa na kusema kukusanyika kwa mamilioni ya wafanyaziara au mazuwar katika sehemu moja kwa wakati mmoja kunatoa fursa ya ukuaji na maendeleo katika nyanja za kijamii, kimaadili, kielimu, kisiasa na nyenginezo.

Ni mkusanyiko ambapo washiriki wote ni sawa na hakuna tofauti au kipaumbele kulingana na rangi, hali ya kijamii, mali, cheo, nk, alisema.

Katika mkusanyiko huu, mtu anaweza kuona mshikamano wa kijamii katika hali yake ya wazi zaidi, Qassim Abdullah aliongeza.

Pia kuna hali ya kiroho yenye nguvu katika msafara huu ambayo huhisiwa na wote wanaoshiriki katika maandamano hayo, alibainisha.

Mwanazuoni huyo aidha ameashiria umuhimu wa matembezi ya Arbaeen katika kuhifadhi ujumbe na thamani za harakati ya Imam Hussein (AS) na kusema matembezi hayo ni hatua ya kuzingatiwa thamani na misingi ambayo Imam Hussein (AS) na masahaba wake waliuawa shahidi katika njia ya kuhuisha Uislamu.

Alisema mageuzi ambayo Imam Hussein (AS) aliyafuata yamedhihirika katika matembezi ya Arbaeen kwani inatoa pahali pa uwezo wa binadamu kudhihirika na kuimarishwa.

Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu  wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdi na jeshi katili la la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.

Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi kubwa ya wasiokuwa Mashia humiminika  katika mji Karbala nchini Iraq, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) ili kushiriki katika shughuli za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala. Arbaeen ya mwaka huu yamefanyika Agosti 25.

Harakati ya mapambano ya Imam Hussein (AS) dhidi ya dhulma na ufisadi wa utawala wa Bani Umayya ilijaa hamasa, kujitolea na kusabilia kila kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, haki na uadilifu, na kwa sababu hiyo imegusa sana nyoyo za Waislamu na hata wapenda haki na kweli wasio Waislamu. Harakati hiyo ya Imam Hussein (AS) inaendelea kuibua vuguvugu na hamasa ya aina yake ndani ya nafsi za wapenzi wa mtukufu huyo.

3489648

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: arbaeen
captcha