IQNA

Mauritania yapanga mashindano ya Qur’ani  na Hadithi Afrika Magharibi

18:27 - September 04, 2024
Habari ID: 3479382
IQNA - Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Mauritania inapanga kuandaa mashindano ya Qur'ani na Hadithi kwa nchi za Afrika Magharibi.

18:27 - 2024/09/04

Wizara ilisema usajili wa shindano hilo umekamilika na kazi imeanza kutathmini sifa za waliojisajili. 

Taarifa hiyo imebaini kuwa ofisi ya mwongozo wa Kiislamu katika wizara hiyo itaendelea na mchakato wa tathmini ya kufuzu hadi Septemba 6.

Ukomo wa umri wa kushiriki katika mashindano hayo ni miaka 15 hadi 50, wizara iliongeza.

Washindani watashindana katika kategoria nne ambazo ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani na Hadithi za Mtume Muhammad (SAW), ilisema.

Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyoko katika eneo la Maghreb magharibi mwa Afrika Kaskazini.

Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa takriban milioni 4 na takriban Wamauritania wote ni Waislamu.

Shughuli na programu za Qur'ani ni maarufu sana katika nchi ya Kiafrika. Nchi hiyo ina utamaduni uliojikita katika  kuhifadhi Qur'ani na idadi kubwa ya wanawake waliohifadhi Qur’ani na Hadith nchini humo haiwezi kulinganishwa na nchi yoyote ulimwenguni .

 

4234805

Habari zinazohusiana
captcha