Hafla hiyo iliyopewa jina la "Kaigrafia ya Qur’ani" imeandaliwa na Idara ya Sanaa ya Umma ya Iraq kwa ushirikiano na Taasisi ya Sanaa ya Kiislamu ya Ibn Bawwab.
Kwa mujibu wa Alsumaria News, maonyesho hayo yanawaleta pamoja waandishi 30 wa kaligrafia kutoka mikoa mbalimbali nchini Iraq, wakionyesha kazi yao ya kuandika kurasa za Qur'ani kwa mtindo wa jadi wa Iraq. Wasanii hawa wamekusanyika ili kuonyesha ujuzi wao wa kipekee katika sanaa ya uandishi wa kaligrafia ya Qur’ani.
Waziri huyo alitoa wito kwa mashirika ya wakfu ya Shia na Sunni ya Iraq kuunga mkono miradi inayohusiana maandishi ya aya za Qur’ani hata kwa idadi ndogo, ili kazi hizi ziweze kuonyeshwa kwenye maonyesho ya mara kwa mara.
Qasem Mohsen, mkurugenzi wa Idara ya Sanaa ya Umma ya Iraq, alisisitiza umuhimu wa tukio hilo: "Maonyesho haya yana umuhimu wa pekee kwa vile yanaangazia kaigrafia ya Qur'ani, ya waanndishi mashuhuri ambao vidole vyao vimeheshimiwa kwa kuandika aya za Qur'ani."
"Kaligrafia ya Qur'ani ina thamani na heshima kubwa miongoni mwa Wairaqi wote," alisema.
Ameongeza kuwa, "Idara ya Sanaa ya Umma inatilia maanani sana tajriba zote za kisanii, hasa zile ambazo zina nafasi kubwa katika nyoyo za Wairaqi, kama vile maonyesho haya ya Qur'ani."
/3490389