Maandamano hayo yalifanyika kwa mwaliko wa kundi la “Action for Palestine”, ambapo washiriki walilaani vikali mashambulizi yanayoendelea dhidi ya raia wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza, hususan wanawake, watoto na wazee wasiokuwa na hatia.
Aidha, waandamanaji walionya dhidi ya kuendelea kuzuiwa kwa misaada ya kibinadamu kuingia Gaza, hali ambayo imeongeza mateso ya wananchi, kwa mujibu wa taarifa ya Kituo cha Habari cha Palestina.
Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa, misaada michache ya kibinadamu iliyoruhusiwa kuingia Gaza chini ya makubaliano ya usitishaji mapigano tangu tarehe 10 Oktoba haijatosha kukomesha njaa wala kupunguza athari zake. Hali hii, sambamba na kudorora kwa uchumi katika eneo hilo, imewanyima wakazi wengi uwezo wa kununua chakula cha msingi.

Waandaaji wa mkusanyiko wa Rabat walisema maandamano hayo yalifanyika kuitikia wito wa harakati ya Hamas, iliyozitaka jamii huru duniani kuandaa maandamano ya kila wiki katika mataifa mbalimbali, kupinga vita vinavyoendelea dhidi ya Gaza.
Habari inayohusiana:
Wakiwa wamebeba bendera za Palestina na mabango ya kuunga mkono watu wa Gaza, washiriki waliinua sauti zao kwa kauli za kuunga mkono muqawama (mapambano ya kujilinda) na kudhihirisha mshikamano wao wa dhati na wananchi wa Palestina, wakisisitiza haki, utu na uadilifu kwa mujibu wa misingi ya ubinadamu na maadili ya Kiislamu.
3496328