al aqsa

IQNA

IQNA – Jordan imetoa onyo kali kwa washirika wake wa kimataifa kwamba utawala haramu wa Israel unaweza kuwa karibu kuchukua udhibiti kamili wa msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa AL Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Habari ID: 3482595   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/08/07

IQNA – Mji mtukufu wa Karbala nchini Iraq unaandaa Kongamano la 5 la Kimataifa la Nidaa al-Aqsa (Wito wa Al-Aqsa).
Habari ID: 3482540   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/26

IQNA – Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa  Palestina, Hamas, imelaani uvamizi wa walowezi wa Kizayuni katika Msikiti wa Al-Aqsa jijini Al Quds (Jerusalem), ikionya kuwa vitendo hivi vya wazi vya uchokozi vitamalizika kwa hasara ya utawala ghasibu wa Israel na walowezi wa Kizayuni.
Habari ID: 3482529   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/24

IQNA-Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi wa Palestina (Hamas) iimelaani vikali uamuzi wa awali wa bunge la utawala wa Israel (Knesset) kupitisha muswada wa mrengo wa kulia wenye nia ya kupiga marufuku wito wa Sala ya Kiislamu (Adhana) kupitia vipaza sauti katika misikiti ya Mji Mkongwe wa al-Quds (Jerusalem) na maeneo mengine yote yaliyovamia na kukaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Habari ID: 3482428   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/02

IQNA – Maelfu ya waumini wa Kiislamu wameadhimisha swala ya Eid al-Adha katika Msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa, katika mji mtakatifu wa Al-Quds, siku ya Jumatano.
Habari ID: 3482290   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/27

IQNA – Utawala dhalimu wa Israel umewapiga marufuku wahubiri wawili mashuhuri wa Kiislamu wa Palestina kuingia katika Msikiti wa Al‑Aqsa  jijini Al Quds (Jerusalem) kwa kipindi cha miezi sita.
Habari ID: 3482211   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/05/07

IQNA – Sheikh Raed Salah na Sheikh Kamal al‑Khatib wamelaani marufuku ya wiki moja iliyowekwa na mamlaka za utawala haramu wa Israel kuwazuia kuingia katika Msikiti wa Al‑Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo, wakisema ni “shambulio dhidi ya dini yetu.”
Habari ID: 3482178   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/04/29

IQNA-Utawala wa Kizayuni wa Israel umewawekea vizuizi vikali Wapalestina kuingia katika Msikiti wa al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) ambao unaukalia kwa mabavu, kwa ajili ya Swala ya Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3481966   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/21

IQNA — Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu ya Palestina imetangaza mpango jumuishi wa kuukaribisha na kuadhimisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika Msikiti wa Al‑Aqsa, uliopo katika mji mtakatifu wa al‑Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel.
Habari ID: 3481954   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/18

IQNA – Utawala ghasibu wa Israel umetangaza mipango ya kuweka vizuizi kwa waumini Waislamu wanaotaka kufika Msikiti wa Al-Aqsa katika mji mtakatifu wa al-Quds (Jerusalem0, wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3481807   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/15

IQNA – Imamu wa Msikiti wa Al-Aqsa amesifu msaada wa Malaysia kwa Palestina na kulaani ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina.
Habari ID: 3481776   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/06

IQNA – Viongozi wa Palestina wamelaani vikali hatua ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kuingia kwa nguvu katika katika eneo la Msikiti wa Al‑Aqsa jijini Quds (Jerusalem) wakati wa sikukuu ya Kiyahudi ya Hanukkah.
Habari ID: 3481673   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/17

IQNA – Qari na Muadhini wa Msikiti wa Al‑Aqsa katika al‑Quds (Jerusalem) ameaga dunia baada ya maisha marefu ya ibada katika Qibla cha kwanza cha Waislamu.
Habari ID: 3481660   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/12/14

IQNA – Sheikh Ekrima Sabri amesema mamlaka za Kizayuni zinapotosha dhana za Kiislamu kwa malengo ya kisiasa, wakati akikabiliwa na kesi mjini al-Quds kwa tuhuma za uchochezi.
Habari ID: 3481536   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/18

IQNA – Takriban walowezi haramu 3,939 Waisraeli waliuvamia msikiti mtukufu wa Al-Aqsa wiki iliyopita wakiwa chini ya ulinzi wa majeshi ya utawala wa Kizayuni, kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni.
Habari ID: 3481489   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/09

IQNA-Itamar Ben Gvir, Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni, licha ya onyo kutoka kwa Waqfu wa Kiislamu, ameuvamia tena Msikiti wa Al-Aqsa jijini Quds (Jerusalem) kwa mara ya pili ndani ya wiki moja.
Habari ID: 3481381   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/18

IQNA – Jumba la Makumbusho moja jijini Istanbul limezindua uzoefu wa hali halisi ya mtandao (Virtual Reality – VR) unaowawezesha wageni kutembelea Msikiti wa Al-Aqsa na mji wa al-Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Israel, kana kwamba wanatembea humo kwa miguu.
Habari ID: 3481339   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/07

IQNA – Mamlaka ya utawala wa Kizayuni imezuia Sheikh Ikrima Sabri, khatibu wa Msikiti wa Al-Aqsa na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la al-Quds (Jerusalem) kuingia na kuswali katika eneo hilo takatifu kwa muda wa miezi sita — hatua iliyolaaniwa vikali kama sehemu ya kampeni ya kuwalenga viongozi wa kidini wa Kipalestina.
Habari ID: 3481336   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/07

IQNA – Polisi wa utawala wa Israel wamemkamata Sheikh Mohammad Sarandah, khatibu wa Msikiti wa Al-Aqsa, muda mfupi baada ya kutoa hotuba ya Ijumaa, kwa mujibu wa Waqfu wa Kiislamu wa al-Quds.
Habari ID: 3481258   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/20

IQNA – Makumbusho ya Kiislamu ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa yanahifadhi mkusanyiko wa kipekee wa nakala nadra za kihistoria za Qur'an Tukufu, kuanzia enzi za Umawiyah hadi Uthmaniyah.
Habari ID: 3481154   Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/29