mazishi ya imam khamenei - Ukurasa 2

IQNA

IQNA – Kuadhibiwa kwa wauaji wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ni wajibu wa kimsingi wa mamlaka ya Jamhuri ya Kiislamu, amesema afisa mwandamizi wa serikali.
Habari ID: 3482455   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/07

IQNA – Mwili mtakatifu wa Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayed Ali Khamenei, utapelekwa katika maeneo matakatifu nchini Iraq kwa ajili ya ziara ya mwisho (ziara ya mazishi), tukio ambalo ni la kwanza la aina yake katika kipindi cha miaka 69.
Habari ID: 3482454   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/07

IQNA – Ayatullah Sayyid Mohammad Reza Sistani, mwana mkubwa wa Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Sistani, ametangaza kuwa kiongozi huyo mkuu wa kidini hataweza kuongoza sala za maiti za Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, nchini Iraq.
Habari ID: 3482453   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/07

IQNA-mamilioni ya waombolezaji leo wameikusanyika katika mji mtakatifu wa Qom nchini Iran tangu asubuhi kushiriki katika mazishi ya Kiongozi Shahidi.
Habari ID: 3482452   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/07

TEHRAN – Katika hali iliyojaa uzito wa kiroho na huzuni kubwa, watoto wa kiume wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, wamehudhuria swala ya mazishi ya baba yao iliyofanyika katika eneo la Sala (Musalla) la Imam Khomeini (RA) jijini Tehran, siku ya Jumapili, Julai 5, 2026. Ibada hiyo iliyojaa unyenyekevu ilitoa fursa kwa familia na waombolezaji waliokuwepo kuungana katika sala za mwisho kwa ajili ya kiongozi huyo ambaye ameacha alama isiyofutika katika uongozi wa Kiislamu na harakati za ukombozi duniani.
Habari ID: 3482451   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/06

TEHRAN – Kwa usiku wa pili mfululizo (Julay 6), umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza katika Ukumbi wa Sala (Musalla) wa Imam Khomeini (RA) jijini Tehran, ili kushiriki katika shughuli za kuaga mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
Habari ID: 3482450   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/06

IQNA-Wakati shughuli za mazishi na kuaga mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, zikiendelea nchini Iran, Waislamu na wafuasi wake nchini Marekani wameungana kufanya ibada za maombolezo kufuatia kuondoka kwa kiongozi huyo.
Habari ID: 3482449   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/06

IQNA- Mamlaka katika Jimbo la Najaf nchini Iraq zimekamilisha maandalizi ya usalama, vifaa, na huduma kwa ajili ya msafara wa mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei.
Habari ID: 3482448   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/06

IQNA – Mufti Mkuu wa Tunisia, Sheikh Hisham Ben Mahmoud, ametoa heshima zake kwa kiongozi shujaa wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, akielezea mwito wake wake  kuhimiza umoja , mshikamano, na uvumilivu miongoni mwa Waislamu kama mwendelezo wa ujumbe wa Mtume Muhammad (SAW).
Habari ID: 3482447   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/06

IQNA-Umati wa waombolezaji umefurika barabarani katika mji mkuu wa Iran huku msafara wa mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, yakianza. Tukio hili linaelezwa na maafisa kama mkusanyiko mkubwa zaidi wa umma kuwahi kushuhudiwa katika historia ya kisasa ya taifa hilo.
Habari ID: 3482446   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/06

IQNA – Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya kupigania ukombozi wa Palestina, amesema kuwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, alikuwa na mapenzi ya dhati kwa Palestina.
Habari ID: 3482445   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/05

IQNA – Naibu Mkuu wa Baraza la Kisiasa la harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa kuuawa Shahidi Ayatullah Seyyed Ali Khamenei kumeongeza mara mbili nguvu ya makundi ya Muqawama wa Kiislamu na watu huru duniani kote.
Habari ID: 3482444   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/05

IQNA – Kiongozi mwandamizi wa Malaysia ameonyesha imani kuwa itikadi alizozisimamia na kuzipigania Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, zitaendelea kuishi na kudumu hata baada ya kuondoka kwake, akisema kuwa Uislamu utaendelea kusonga mbele kupitia mwongozo na msukumo wa kiongozi huyo.
Habari ID: 3482443   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/05

IQNA – Video ya wimbo wa kishujaa wenye jina la “We Must Rise” (Lazima Tuinuke) imetolewa rasmi kwa lugha ya Kiingereza ambapo muimbaji ni Mahdi Dardashtian. Wimbo huu ni kazi iliyosikika kwa sauti za huzuni katika majilisi za maombolezo katika majimbo mbalimbali nchini Marekani wakati wa usiku wa mwezi mtukufu wa Muharram. Kazi hii imedhihirisha mshikamano wa kina wa nyoyo za watu kutoka mataifa tofauti; watu waliojitokeza kuomboleza msiba wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuonyesha mshikamano wa dhati na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Hili ni dhihirisho tosha kuwa huzuni hii haijafungwa na mipaka ya kijiografia, bali inagusa nyoyo za watu huru ulimwenguni kote, ikionyesha kuwa mapenzi kwa shakhsia wa haki hayajui mipaka.
Habari ID: 3482442   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/05

IQNA – Ibada ya kuaga mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei (Mwenyezi Mungu awe radhi naye), imeendelea kwa siku ya pili leo tarehe 5 Julai 2026, katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini (RA) uliopo Tehran. Mji wa Tehran umezama katika majonzi mazito huku mamilioni ya waombolezaji wakimiminika katika eneo la Musalla ili kutoa heshima za mwisho kwa shakhsia huyu mahiri na mlinzi wa Ummah. Hali ya huzuni imetawala kote, huku nyoyo za Waislamu zikiwa zimejaa msiba mkubwa wa kuondokewa na kiongozi wao shujaa aliyesimamia haki dhidi ya dhulma za ulimwengu.
Habari ID: 3482441   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/05

IQNA-Mamilioni ya waombolezaji wameshiriki Swala ya maiti ya mwili mtakatifu wa Imam shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na kundi la wanafamilia wake watukufu iliyofanyika kwa uwepo mkubwa wa viongozi wa serikali, jeshi na umma kwa ujumla.
Habari ID: 3482440   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/05

IQNA – Rais wa Baraza la Ushauri la Mashirika ya Kiislamu ya Malaysia (MAPIM) amesema kuwa mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, yanatoa ujumbe mzito unaovuka mipaka ya Iran.
Habari ID: 3482438   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/04

IQNA-Viongozi waandamizi wa Iran, marais na wakuu wa nchi, pamoja na wageni mashuhuri na wajumbe wa ngazi za juu kutoka mataifa mbalimbali duniani, wamefika Tehran kutoa heshima zao kwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.
Habari ID: 3482437   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/04

IQNA – Tangu alfajiri ya jana, Julai 3, jijini Tehran, kumekuwa na mwendelezo wa shughuli za heshima za mwisho kwa mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyed Ali Khamenei, na mashahidi wengine waliojitoa mhanga kwa ajili ya Uislamu na taifa la Iran. Shughuli hii muhimu inafanyika katika Musalla wa Imam Khomeini (RA).
Habari ID: 3482436   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/04

IQNA-Mamilioni ya waumini wanatarajiwa kufurika katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala nchini Iraq kushiriki katika shughuli za mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.
Habari ID: 3482433   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/03