Nasrallah pia alisema kuwa kumiminwa silaha wa nchi za Magharibi ili kuilinda Israel dhidi ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ni dalili wazi ya Tel Aviv kutokuwa na uwezo wa kujilinda.
"Israel haina nguvu kama ilivyokuwa kabla ya vita hivi, na hadhi na uwezo wake wa kijeshi hauko tena kama ulivyokuwa," alisema.
Sayyid Nasrallah alisema hayo jana kwenye hotuba ya kumuenzi shahid Fuad Ali Shukr, mmoja wa makamanda wa ngazi za juu wa Hizbullah ya Lebanon aliyeuawa kigaidi na Wazayuni wiki iliyopita.
Amesema kuwalenga viongozi wa Hizbullah hakutadhoofisha azma na irada ya harakati hiyo ya kuendelea na njia yake, akisisitiza kwamba mauaji ya hivi karibuni hayatabadilisha dhati na asili ya msingi ya muqawama.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, mauaji ya hivi karibuni ya viongozi wa muqawama yamezidisha masaibu ya utawala ghasibu wa Israel, na hivyo kuchochea ongezeko la operesheni dhidi ya Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kukimbia Wazayuni kutoka maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, wakihofia ulipizaji kisasi kutoka kwa Iran na Hizbullah.
Sayyid Nasrallah ameeleza bayana kuwa, utawala wa Kizayuni unapasa kusubiri majibu makali kutoka kwa kambi ya muqawama na kuongeza kuwa, hakuna shaka mrengo wa mapambano utapa ushindi.
3489412