Diplomasia
TEHRAN (IQNA) – Rais wa Iran Ebrahim Raisi, ambaye yuko katika safari rasmi nchini Syria, ametembelea kaburi takatifu la Bibi Zainab (SA) huko Damascus.
Habari ID: 3476956 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/04
Diplomasia
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Iran ameashiria kukasirishwa utawala wa Kizayuni kufuatia kuhuishwa uhusiano kati ya Iran na Saudia na akasema: Maadui khususan utawala wa Israel wamekasirishwa na hatua hii na sababu yake ni njama wanazofanya za kueneza migawanyiko.
Habari ID: 3476951 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/03
Diplomasia
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, serikali ya Syria pamoja na wananchi wa nchi hiyo wamepitia masaibu na matatizo mengi na hii leo taifa hilo limeweza kupata ushindi.
Habari ID: 3476950 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/03
Maoni
TEHRAN (IQNA)- Jana, tarehe 10 Ordibehest, 1402 Hijria Shamsia sawa na Aprili 30, ilikuwa siku ya kumbukumbu ya kufukuzwa wakoloni wa Kireno katika maji ya Kusini mwa Iran hapo mwaka 1622, na inatambuliwa nchini Iran kuwa Siku ya Kitaifa ya Ghuba ya Uajemi.
Habari ID: 3476942 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/05/01
Mhimili wa Muqawama
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Ijumaa alionana na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah na kujadiliana naye masuala muhimu ya pande mbili, ya kieneo na ya kimataifa.
Habari ID: 3476931 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/29
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, jamii ya wafanyakazi wa viwandani haijakubali kutumiwa vibaya na adui na wanaolitakia mabaya taifa la Iran.
Habari ID: 3476930 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/29
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran anasema ukombozi wa Palestina na mwisho wa hali ya janga ambalo Wapalestina wanakabiliwa nalo unakaribia kwani utawala wa Kizayuni wa Israel unaonekana kuwa dhaifu kuliko hapo awali.
Habari ID: 3476928 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/28
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian
TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza azma yake katika kadhia ya Palestina na kusema itaendelea kuwaunga mkono wanamapambano wa Palestina katika kukabiliana na vitendo vya kichokozi vya utawala wa Kizayuni.
Habari ID: 3476906 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/24
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Ebrahim Raisi, ameuonya vikali utawala wa kibaguzi wa Israel kuhusu kuchukua hata hatua ndogo ya uchokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, akisema Iran itajibu uchokozi huo kwa "kuangamiza Haifa na Tel Aviv."
Habari ID: 3476884 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/18
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa iwapo hatua za kimantiki zitachukuliwa, inawezekana kushindwa mahesabu ya adui
Habari ID: 3476877 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/16
Ukombozi wa Palestina
TEHRAN (IQNA)- Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yamefanyika katika kila pembe ya Iran ya Kiislamu kwa kauli mbiu kuu "Palestina mhimili wa umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu; Quds inakaribia kukombolewa".
Habari ID: 3476864 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/14
Ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Quds
TEHRAN (IQNA)-Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekumbusha wajibu wa kisheria wa mashirika na taasisi za kimataifa na za kutetea haki za binadamu wa kuunga mkono haki za watu walio chini ya utawala ghasibu huko Palestina, na kutoa wito wa kukomeshwa uvamizi huo na kusimamisha jinai za Wazayuni.
Habari ID: 3476862 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/13
Rais wa Iran
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi amesema: taifa adhimu la Iran litatangaza kwa mara nyingine tena kwamba litabaki kuwa thabiti katika malengo ya Uislamu hadi itakapokombolewa Quds kikamilifu, kwa kushiriki kwa wingi katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds.
Habari ID: 3476859 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/13
Mashindano ya Qur'ani
TEHRAN (IQNA) – Yunes Shahmoradi kutoka Iran aliyeshika nafasi ya kwanza katika Toleo la 2 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Otr Elkalam nchini Saudi Arabia amesema shindano hilo lilikuwa la kiwango cha juu.
Habari ID: 3476843 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/10
Mashidano ya Qur'ani
TEHRAN (IQNA) - Ifuatayo ni qiraa ya Qari Yunes Shahmoradi kutoka Iran ambaye aliibuka mshindi katika toleo la pili la Shindano la Kimataifa la Qur’ani Tukufu la Otr Elkalam nchini Saudi Arabia.
Habari ID: 3476838 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/09
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amefanya mazungumzo ya simu na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na kutoa wito wa kuitishwa kikao cha dharura cha jumuiya hiyo ili kukabiliana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa.
Habari ID: 3476835 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/08
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeitisha mkutano wa dharura kujadili hali ilivyo katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, baada ya askari wa utawala haramu wa Israel kuvamia Msikiti wa al-Aqsa mjini Quds (Jerusalem) na kuwalenga waumini wa Kipalestina kwa guruneti.
Habari ID: 3476827 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/07
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hujuma na shambulio la kinyama la vikosi vya utawala ghasibu vya Kizayuni dhidi ya waumini wa Kipalestina waliokuwa katika ibada ya itikafu katika msikiti wa Al-Aqsa kwa mara nyingine imeweka bayana sura ya kinyama na kikatili ya utawala huo na ukiukaji wa haki za binadamu.
Habari ID: 3476814 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/05
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, matukio ya kisiasa ulimwenguni yamekuwa yakitokea kwa kasi na wakati huo huo yamekuwa katika mkondo wa kudhoofisha kambi ya maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3476813 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/05
Ukombozi wa Palestina
TEHRAN (IQNA)- Mwenyekiti wa Makao Makuu ya Intifadha na Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Iran amesema nara na kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa Quds mwaka huu ni : "Palestina ni mhimili wa Umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu na Quds (Jerusalem) Inakaribia Kukombolewa."
Habari ID: 3476811 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/04/04