iqna

IQNA

IQNA-Kiongozi mmoja wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amejibu matamshi ya kijuba ya rais wa Marekani, Donald Trump aliyetan gaza nia ya Marekani ya kuuteka Ukanda wa Gaza na eti kuugeuza kuwa eneo huru, akimwambia, Ghaza si bidhaa ya kupigwa mnada.
Habari ID: 3480691    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/16

IQNA- Mkuu wa Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO) amesema kuwa mazungumzo kati ya nchi za Kiislamu ni hitaji lisiloweza kuepukika katika kutatua changamoto za msingi za ubinadamu.
Habari ID: 3480688    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/15

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameutaka Ulimwengu wa Kiislamu kutoruhusu suala la Palestina lisahaulike akisisitiza ulazima wa kukabiliana na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.
Habari ID: 3480666    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/10

IQNA-Sayyid Abdul-Malik Badr al-Din al-Houthi, Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameeleza kuwa, jamii za Kiarabu na Umma wa Kiislamu zinabeba dhima ya msingi kuhusu mauaji ya kimbari yanayoendelea kutekelezwa na utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Wapalestina huko Gaza akisisitiza matokeo mabaya ya kutochukua kwao hatua.
Habari ID: 3480658    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/09

IQNA – Utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakalia ardhi za Palestina kwa mabavu umejaribu mbinu mbalimbali kuiba hati za kale za Kiislamu.
Habari ID: 3480640    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/05

IQNA – Mbio za Marathon za London zilikumbwa na vurugu baada ya waandamanaji kuitaka serikali ya Uingereza kuweka vikwazo kamili vya biashara dhidi ya Israel. 
Habari ID: 3480606    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/28

IQNA – Iran imetan gaza kuwa itawapokea kwa mikono miwili wasomi na wanafunzi wa Kipalestina katika vyuo vikuu vya Iran kufuatia uharibifu mkubwa wa taasisi za elimu katika Ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi ya utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3480542    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/15

IQNA – Maelfu ya Wamoroko walikusanyika Jumapili katika mji mkuu, Rabat, kuonyesha mshikamano wao na watu wa Palestina na kulaani uhalifu unaoendelea wa utawala katili wa Israel katika Ukanda wa Gaza. 
Habari ID: 3480541    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/14

Jinai za Israel
IQNA-Umoja wa Mataifa umesema wanawake na watoto wa Kipalestina ndio pekee waliouawa katika mashambulizi yapatayo 36 ya anga yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza tangu katikati ya mwezi Machi na kuonya kwamba mashambulizi ya kijeshi ya Israel yanahatarisha "kuendelea kuwepo Wapalestina kama jamii".
Habari ID: 3480529    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/12

IQNA – Waislamu nchini Singapore (Singapuri) wamejitolea kuchangia nyama kwa watu wa Gaza wakati wa sikukuu ya Idul Adha, kutokana na janga la kibinadamu katika Ukanda huo uliozingirwa na utawala dhalimu wa Israel.
Habari ID: 3480526    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/11

IQNA-Shirika moja la kimataifa limelaani hatua ya kampuni ya Microsoft ya Marekani kumfuta kazi mhandisi wa programu mwenye asili ya Morocco, Ibtihal Aboussad, ambaye aliandamana hadharani kupinga uungwaji mkono wa kampuni hiyo kwa utawala katili wa Israel wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Microsoft.
Habari ID: 3480521    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/10

IQNA-Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina , Hamas, imelinganisha vitendo vya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza na mauaji ya kimbari ya Rwanda, huku ikisifu hatua ya Umoja wa Afrika Afrika kumfukuza balozi wa utawala wa Israel kutoka mkutano maalum wa kumbukumbu uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia.
Habari ID: 3480514    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/08

IQNA-Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmed al-Khalili, amekosoa vikali kimya kinachoonyeshwa mbele ya jinai za kinyama zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3480497    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/05

IQNA – Mashambulizi ya anga ya utawala katili wa Israel katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 100, wakiwemo 33 waliokuwa wakijisitiri katika shule.
Habari ID: 3480492    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/04

IQNA – Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limeripoti kuwa zaidi ya watoto 300 wameuawa Gaza tangu vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel vilipoanza upya vita mnamo Machi 18.  
Habari ID: 3480484    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/02

IQNA- Swala ya Ijumaa ya mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani katika misikiti mbalimbali duniani, ikiwemo Msikiti wa Masjid al Al-Haram katika mji mtakatifu wa Makka, na Msikiti wa Al-Azhar nchini, iliandamana na dua kwa ajili ya Wapalestina wa Gaza na Msikiti wa Al-Aqsa.
Habari ID: 3480464    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/29

IQNA – Jiji la Vienna, mji mkuu wa Austria, lilishuhudia maandamano makubwa yanayopinga kuendelea kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza. Waandamanaji walibeba mabango na vipeperushi vyenye maandiko, “Acha kuua watoto,” “Acha vita sasa,” na “Susia Israel."
Habari ID: 3480427    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/24

IQNA-Vikosi vya Jeshi la Yemeni vimetan gaza shambulio jingine dhidi ya vikosi vya Marekani katika eneo la Bahari ya Shamu, vikitumia makombora na ndege zisizo na rubani ili kuzuia shambulio tarajiwa la Marekani dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.
Habari ID: 3480393    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/18

IQNA – Harakati ya Ansarullah ya Yemen imeahidi kujibu uchokozi wa kijeshi wa hivi karibuni wa Marekani, kufuatia mashambulizi ya angani ya Marekani na Uingereza ambayo yalilenga maeneo kadhaa kote nchini, ikiwemo mji mkuu, Sanaa, na jimbo la kaskazini la Saada.
Habari ID: 3480380    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/16

IQNA-Mufti Mkuu wa Oman amewataka Waislamu wote na watu wanaopenda uhuru duniani kusaidia watu wanaodhulumiwa wa Gaza wanaoishi katika hali mbaya.
Habari ID: 3480336    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/09