IQNA

Al-Azhar Kuandaa Shindano la Kuhifadhi Qur’ani kwa Wanafunzi

22:37 - January 05, 2025
Habari ID: 3480006
IQNA - Chuo Kikuu cha Al-Azhar cha Misri kimetangaza shindano la kuhifadhi Qur’ani miongoni mwa wanafunzi wake katika vitivo vya chuo hicho jijini Cairo na maeneo mengine ya nchi hiyo.

Rais wa chuo hicho, Sheika Salama Daoud, alisema shindano hili limeandaliwa mahsusi kwa wanafunzi wa kiume na wa kike wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar jijini Cairo na maeneo mbalimbali ya Misri, ambapo zawadi za thamani zimepangwa kutolewa kwa washiriki bora. Mwisho wa shindano hili, mshindi wa kwanza atapokea pauni 100,000 za Misri, mshindi wa pili atapewa pauni 75,000 za Misri, na mshindi wa tatu atapewa pauni 50,000 za Misri, alibainisha.

Sheikh Daoud amesema shindano hili ni fursa ya dhahabu kwa wanafunzi wa kiume na wa kike kuonyesha vipaji vyao katika kuhifadhi Qur’ani na kushindania zawadi za pesa za thamani. Uongozi wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar umeeleza masharti ya ushiriki, ukiweka wazi kuwa uelewa wa dhana za Qur’ani na Asbab al-Nuzul (sababu za kueteremka aya) za aya hizo ni miongoni mwa masharti haya. Imesema kuwa kuhamasisha wanafunzi kupiga hatua katika kuhifadhi Qur’ani na kuimarisha maadili ya kidini na kiroho miongoni mwao ni miongoni mwa malengo ya shindano hili.

3491325

Habari zinazohusiana
Kishikizo: al azhar qurani tukufu
captcha