Afisa huyo wa Saudia ametoa salamu za rambirambi kwa kufa shahidi Rais wa Iran Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian na wenzake ajali ya hivi karibuni ya helikopta na alitakia taifa la Iran na serikali afya na mafanikio.
Vile vile amezungumzia msimu ujao wa Hijja na kusema nchi yake imechukua hatua zote muhimu kwa ajili ya Hija yenye mafanikio.
Mjumbe huyo wa Iran kwa upande wake ameishukuru Saudi Arabia kwa kutuma ujumbe na kutoa salamu za rambirambi kwa njia ya simu baada ya kufa shahidi rais wa Iran na wenzake.
Enayati pia ameitaja Hija kuwa ni dhihirisho la umoja wa Waislamu na akasisitiza ushirikiano wa nchi hizo mbili kutekeleza ibada ya Hija ya Waislamu.
Jumla ya Mahujaji 87,550 kutoka Iran watashiriki katika ibada ya Hija ya mwaka huu.
Hija ni safari ya kwenda katika mji mtakatifu wa Makka ambayo kila Mwislamu mwenye na uwezo wa kimwili na kifedha analazimika Kuhiji angalau mara moja katika maisha yake.
Hija ya kila mwaka inachukuliwa kuwa moja ya nguzo za Uislamu na ni dhihirisho la umoja wa Waislamu na kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu.
3488518