IQNA

Jamii ya Qur’ani ya Iran yahuisha kiapo cha utiifu kwa njia ya Shahidi Imam Khamenei

17:17 - March 07, 2026
Habari ID: 3482023
IQNA – Mkutano wa wanachama wa jamii ya Qur’ani nchini Iran umefanyika mjini Tehran siku ya Jumamosi.

Katika mkusanyiko huo, umefanyika katika Uwanja wa Abuzar mbele ya Msikiti wa Abuzar, wanazuoni, wasomaji na wanachama wa jamii ya Qur’ani wamehuisha kiapo chao cha utiifu kwa njia na misingi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei.

Katika hafla hiyo pia, baadhi ya maqari mashuhuri wa kimataifa wamesema aya za Qur’ani Tukufu.

Msikiti wa Abuzar ni miongoni mwa misikiti ya Tehran ambayo iliharibiwa na kuchomwa moto na watu waliokuwa na uhusiano na Marekani na utawala wa Kizayuni wakati wa ghasia za hivi karibuni nchini humo.

Aidha, msikiti huo ndio mahali ambapo jaribio la kumuua Ayatullah Khamenei lilifanyika mwaka 1981.

Kwa zaidi ya miongo mitano iliyopita, msikiti huo umekuwa kitovu cha matukio makubwa ya Qur’ani na vikao vya ufundishaji wa Qur’ani, ambapo walimu wengi mashuhuri wa Qur’ani, wahifadhi na wasomaji hodari wamelelewa na kuandaliwa kupitia vikao hivyo.

Marekani pamoja na utawala wa Israel walianzisha mashambulizi dhidi ya Iran kuanzia asubuhi ya Jumamosi, tarehe 28 Februari.

Kujibu uchokozi huo wa Marekani na Israel—uliopelekea kuuawa shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam  Seyed Ali Khamenei, pamoja na makamanda kadhaa wa ngazi za juu za kijeshi na mamia ya raia—Iran ilianzisha Operesheni Ahadi ya Kweli 4 (True Promise 4), ikifanya mashambulizi makubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya malengo ya Israel na kambi za Marekani katika eneo hilo.

4338847

Habari zinazohusiana
Kishikizo: imam khamenei shahidi
captcha