Kwa mujibu wa taarifa, vituo 250 vya Qur'ani vitawekwa katika majimbo 12 ya nchi hiyo ya Kiarabu, yakiwemo Basra, Kirkuk, Baghdad na Diyala.
Vituo hivyo vitazinduliwa kwa ushirikiano na Jumuiya ya Wanaharakati wa Qur'ani na kwa usaidizi wa mashirika mengine, taasisi na misikiti.
Wanatoa programu na huduma tofauti za Qur’ani ikijumuisha mafunzo kuhusu usomaji sahihi wa Qur’ani Tukufu.
Wafanyaziara wanaweza pia kuboresha ujuzi wao wa kukariri Kurani katika vituo vya Kurani, kulingana na maafisa wa Kituo cha Dar ul Quran.
Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdi na jeshi katili la la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.
ila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi kubwa ya wasiokuwa Mashia humiminika katika mji Karbala nchini Iraq, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) ili kushiriki katika shughuli za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala. Arbaeen ya mwaka huu inatarajiwa kuanguka mnamo Agosti 25, kulingana na kuonekana kwa mwezi.
Harakati ya mapambano ya Imam Hussein (AS) dhidi ya dhulma na ufisadi wa utawala wa Bani Umayya ilijaa hamasa, kujitolea na kusabilia kila kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, haki na uadilifu, na kwa sababu hiyo imegusa sana nyoyo za Waislamu na hata wapenda haki na kweli wasio Waislamu. Harakati hiyo ya Imam Hussein (AS) inaendelea kuibua vuguvugu na hamasa ya aina yake ndani ya nafsi za wapenzi wa mtukufu huyo.
3489466