IQNA

Shughuli za Qur'ani

Misri yazindua vikao vya Qur’ani kwa wanawake

21:54 - August 18, 2022
Habari ID: 3475641
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Wakfu ya Misri imezindua vikao maalumu Qur'ani kwa wanawake katika majimbo manne ya nchi hiyo kwa mara ya kwanza.

Waziri wa Wakfu Sheikh Mohammed Mukhtar Gomaa vikao hivyo vya kujifvunza Qur’ani inafanyika katika majimbo ya Al-Sharqia, Alexandria, Manoufia na Gharbia.

Vikao hivyo vinafanyika kila wiki siku ya Jumamosi kwenye sehemu za wanawake za misikiti na kumbi za Sala.

Wataalamu wa Qur'ani, walimu na waliohifadhi Qur’ani pamoja na wahubiri wa kidini wanashiriki katika vikao hivyo vya Qur'ani.

Gomaa alisema ni sehemu ya juhudi za wizara hiyo kukuza Quran, kuhimiza wanaharakati wa Qur'ani na kuimarisha nafasi ya wanawake katika jamii.

Wizara hiyo ilisema inapanga kuzindua programu sawa na hizo za Qur'ani kwa wanawake mjini Cairo na baadhi ya majimbo mengine pia.

Baada ya kupunguzwa vizuizi vya corona nchini Misri miezi michache iliyopita, Wizara ya Wakfu  imeanza tena shughuli na programu za Qur’ani katika misikiti na vituo vya kidini kote nchini.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu wanachukua karibu asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo na shughuli za Qur'ani hufanyika kwa wingi katika nchi hiyo.

3480140

Kishikizo: misri ، qurani tukufu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha